January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serengeti kivutio namba moja cha watalii Barani Afrika

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Jarida la The Rolla daily news la nchini Marekani limeitangaza Mbuga ya Serengeti kuwa kivutio namba moja cha watalii Barani Afrika.

Katika Jarida hilo Ngorongoro imeshika nafasi ya saba na kufanya jumla Tanzania kuingiza mbuga mbili katika nafasi hizo kumi.