Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia
Prof.Adolf Mkenda ametangaza kubadilishwa kwa tarehe ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 na Mitaala iliyoboreshwa,kuwa ni Februari Mosi mwaka huu badala ya Januari 31,2025 baada ya kukamilika kwake na kuidhinishwa kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.
Rais Dkt.Samia Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Maboresho ya Sera hiyo jijini Dodoma ambayo ni maelekezo yake aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kufanya mapitio ya Sera ya elimu na Mafunzo ya 2014 pamoja na kufanya maboresho ya mitaala ya elimu katika ngazi mbalimbali ili ijikite katika kutoka elimu ujuzi badala ya elimu ya taaluma pekee.
Prof.Mkenda alisema tayari wageni mbalimbali wameshaanza kuwasili jijini Dodoma kwa ajili ya shughuli hiyo kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Amesema kukamilika kwa sera hiyo na mitaala yake iliyochukua muda wa miaka mitatu kufanyiwa mapitio na marekebisho kunakwenda kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini na utekelezaji wake utakwenda kwa awamu.
“Baada ya maelekezo ya Rais wetu, kazi ilianza, ya kufanya mageuzi na mapitio ya sera na vilevile mapitio ya mitaala, kazi iliyochuyokua takribani miaka mitatu, kazi hii ilifanywa kwa namna shirikishi, kwa kushirikisha wadau mbalimbali, watalam wa elimu, walimu, wanafunzi, wananchi na maoni yalikuwa yakikaribishwa nyakati zote kwa ajili ya kupata namna ya kusonga mbele,”amesema Prof. Mkenda.
“Napenda kuwaarifu kuwa kazi ya kupitia sera ilikamilika, sasa tunayo sera ya elimu haoa nchini ambayo inaitwa kwa kirefu Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023, na sera hiyo imesha idhinishwa na Rais Samia, kupitia kikao cha baraza la mawaziri.
Aidha amesema sambamba na Sera, mitaala nayo imefanyiwa mapitio ili kuendana na sera ambayo wanayo hivi sasa. “Tuna mitaala mipya ambayo tunaitekeleza kwa awamu, suala hili ni kubwa, mageuzi yaliyoko kwenye sera ni makubwa sana yanatekelezwa kwa awamu na tutakuwa tunaona kila mwaka hatua ambazo zinachukuliwa,”amesisitiza waziri.
“Ukienda kwenye sera utaona masuala ya Tehama na mambo yote yanayohusiana na Tehama yalivyozungumzwa, na ukija kwenye mitaala utaona utekelezaji wake unavyofanyika na kuna suala kubwa sana la sayansi, teknolojia, uhandisi na Hisabati ambavyo vinazungumzwa sana kwa haki na kuelekeza kwamba wanatakiwa wafanye nini.
Amesema viongozi wakuu na wandamizi wa nchi wamealikwa na watashiriki katika tukio hilo na wadau mbalimbali wakiwemo sekta ya elimu pia kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya elimu.
“Tunawalika watanzania wote wale watakaokuja wajiandikishe kwasababu tumetoa fulsa, ya kujisajili kushiriki hivyo tunatarajia watafanya hivyo mapema,pia tunawaalika watanzania wote kufuatilia kwenye vyombo vya habari shughuli ya uzinduzi huo ambapo taarifa itatolewa,”amesema Prof.Mkenda.
More Stories
TARURA Kilindi kutumia bil.5.2 bajeti 2025/26
Madiwani Kilindi wapitisha bil.36.8 bajeti 2025/26
THBUB yatoa tamko kulaani mauaji ya Jumanne Juma