January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Senzo aweka wazi mchakato wa mabadiliko Yanga

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha, ameweka wazi mchakato wa kuelekea kwenye mabadiliko ndani ya timu hiyo kuwa, unaendelea vizuri na ambacho kipo kwa sasa ni kuweza kukamilisha suala zima la uchaguzi.

Hata hivyo, amebainisha kuwa jambo ambalo linatazamwa kwa ukaribu kabla ya uchaguzi ni kukamilika kwa usajili wa matawi na wale ambao watakamilisha usajili wao watakabidhiwa vyeti.