November 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Selemani:Bado waajiri hawazingatii sheria na miongozo ya kazi

Na Idd Lugendo,timesmajira

IMEELEZWA kuwa licha ya Tanzania kuwa na  sheria ,sera ,miongozo na kanuni mbalimbali ambazo zipo katika kulinda haki za waajiriwa lakini bado kumekuwa na baadhi ya waajiri wasiozingatia  sheria na miongozo hiyo

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wakili Renatha Selemani amesema kutokana na sheria kuwa na mapungufu  kadhaa kupitia mradi  wa wanawake  na ajira ni unaotekelezwa na shiriika la Bright Jamii Initiative na WilLDAF Tanzania kwa ufadhili kutoka Legal Service Facility waliweza kufanya mapitio mbalimbali ya sheria na kuweza kutoa mapendekezo yao ya maboresho ya sheria hizo

Amesema kufanyika kwa maboresho hayo ni kuleta usawa na haki kazini ambapo katika utekelezaji wa mradi huo wameshirikiana kwa ukaribu  na utatu unaosimamia masuala ya Ajira ambao ni vyama vya wafanyakazi, vyama vya waajiri pamoja na serikali.

Amesema mradi wao ni wa miaka miwili na ulianza kutekelezwa Oktoba 2019 na utakamilika Oktoba 2021 ambapo umetekelezwa katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema lengo la mradi huo ni  kuboresha hali ya maisha ya vijana na Wanawake walioajiriwa katika sekta ya viwanda.