Na Joyce Kasiki, TimesMajira,Online Dodoma
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema mara baada kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekobdari ya mfano ya Iyumbu jijini hapa utasaidia kuchukua wanafunzi wengi zaidi watakaoanza kidato cha kwanza mwakani.
Amesema tangu Serikali ilipopitisha utaratibu wa elimu bila malipo kunekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaopata fursa ya kuandikishwa shule na hivyo kuongeza mahitaji ya shule na vyumba vya madarasa.
Kipanga ameysema hayo jana katika ziara yke ya kukagua maendeleo ya ujenzi ya shule hiyo ya mfano inayojengwa jijini hapa ambayo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi wapatao 1,000.
Amesema katika eneo la Iyumbu Serikali inajenga shule ya mfano kwa gharama ya sh. bilioni 17.1, huku akisema ujenzi wa shule hiyo ni vyema ukamilike mapema kabla ya Februari, mwakani ili wanafunzi watakochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza waanze kuitumia shule hiyo.
“Naagiza ujenzi ikamilike Desemba Ili Januari wanafunzi wadahiliwe kwa ajili ya kuanza masomo,” amesema na kuongeza;
“Ujenzi huu ni kielelezo kuwa Serikali inawajali wananchi wake na kutoa kipaumbele katika suala la elimu.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo,Naibu Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Geoffrey Ngole, amesema ujenzi huo ulianza Julai 2020 na unatarajiwa kukakamilika Februari mwaka 2022 kwa mujibu wa mkatba wa ujenzi.
Hata hivyo amesema wamepokea maagizo ya Serikali ya kukamilisha ujenzi huo kabla ya Februari, huku akisema wataongeza nguvu ili kuhakikisha hilo linatekelezeka.
Amesema ujenzi huo huko katika sehemu tano ikiwemo jengo Kuu, bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 na bweni la wavulana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500, bwalo, nyumba 10 za
watumishi,jengo la Utawala, nyumba za walimu, viwanja vya michezo na matanki ya maji.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Kipanga amesema Serikali imetimiza azma yake kwa kujenzi Chuo cha Ufundi cha Kanda ya Kati na kitakapokamilka kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,000. Awamu ya kwanza kitachukua wanafunzi 1,500.
Amesema Serikali imetoa Sh bilioni 17.9 na Kazi ya Ujenzi ikianza Juni 19,mwaka huu na itachua miezi 18.
Amesema lengo la Chuo hicho ni kuwezesha vijana wengi kupata ujuzi,
kuzalisha vijana wenye ujuzi wa kati.
Amesema Serikali imejipanga kujenga vyuo vya ufundi katika kanda zote ikiwemo kanda ya Kati, kanda ya ziwa, kanda ya Kusini na kanda ya Kaskazini.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi