March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekondari ya Juhudi yafanya ziara Bungeni Dodoma

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online

WANAFUNZI 73 pamoja na walimu sita wa shule ya sekondari Juhudi iliopo wilayani Ilala mkoani Dar-es-Salaam wamefanya ziara ya masomo ya kujifunza shughuli za Bunge katika kikao cha 43 jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya sekondari Juhudi Happynes Pallangyo,amesema ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya shule hiyo ya wanafunzi wake kujifunza kwa vitendo.

“Tumeshiriki kikao cha Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 19, mimi na wanafunzi wangu tumeweza kujifunza mambo mbalimbali na kupata historia pamoja na kazi mbalimbali zinazofanywa na Bunge,”amesema Pallangyo.

Sanjari na hayo, amesema kwa mwaka 2025 ufaulu wa shule hiyo umeongezeka ambapo jumla ya wanafunzi 342 walifanya mtihani wa kidato cha sita kati yao wanafunzi 341 walifaulu.

Ambapo daraja la kwanza walipata wanafunzi 52 ,daraja la pili 185, daraja la tatu wanafunzi 100 na daraja la nne wanafunzi watatu.

Amesema lengo ni kuondoa daraja sifuri ambapo shule imefanikiwa kuongeza ufaulu katika masomo ya kiingereza,kiswahili,jiografia na uchumi.