Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
KIKUNDI cha Vikoba cha Sehundofe Group cha wilayani Ilala kwa kipindi cha miaka 15 kimepata faida ya shilingi milioni 213,386,154,5 .hisa za Wanachama walizokuwa wanaweka akiba.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa Vikoba wa kutimiza miaka 15 Mkurugenzi wa Sehundofe Gruop Semeni Mtoma , amesema kikundi cha Sehundofe Gruop kilianzishwa mwaka 2009 kikiwa na wanachama 21 wanaume watatu na wanawake 18 kwa sasa Sehundofe kina wanachama 758 kati yao wanaume 149 wanawake 609.
“Kikundi cha Sehundofe kilianza na Hisa 120,000/= jamii 21000/= na Faini 3500 /= mpaka mwezi wa September 2024 wameweza kuwekeza kiasi cha shilingi bilioni 2.9 na wameweza kununua jamii yenye thamani ya shilingi milioni 3.3 na wamekopesha mikopo ya shilingi bilioni 4.2 na faida waliopata kwa miaka 15 shilingi milioni 213 ,386,154,5 .alisema “Semeni
Mkurugenzi huyo ,amesema kikundi cha Sehundofe kina wanachama kutoka sehemu mbalimbali Jimbo la Ukonga, nje ya Jimbo la Ukonga,nje ya Dar es Salaam na nje ya Nchi .
“Tunaimani na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutupa uhuru watanzania wenye kipato kidogo kuweza kujiunga wenyewe na kujikwamua kiuchumi katika kuunga mkono Tanzania ya Uchumi wa Viwanda “amesema
Mtoka ,amesema hawana lawama kwenye mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri ya jiji kwasababu wameweza kujisimamia wenyewe kwa kufuata taratibu na sheria walizopewa Mwanasheria wao kwa mikopo wanayokopeshana hivyo hawana budi kuomba mikopo mingine.
Aidha amesema katika miaka 15 ya kikundi hicho wameweza kusaidia shughuli za kijamii shule Msingi Jeshini, wamechangia ujenzi wa choo kwa ajili ya watoto wenye Mahitaji maalum, Shule ya msingi Jica ,wamechangia madawati, shule ya msingi Magorofani ujenzi wa kisima cha maji .
Pia amesema misaada mingine wameweza kutoa nyumba za Ibada msikiti wa Bwela wamechangia Sement, madrasa ya Bwela wamechangia tofali,madrasa ya Mwembeni wamechangia Tofali na Kanisa la KKKT Majohe wamewachangia Wajane, Anglikana wamechangia ujenzi, Viwege TAG wamechangia Sement ,TAG kwa mchumgaji Makuranga Sement,Kanisa Katoliki Mji Mpya Relini ujenzi wa choo ,Yombo Vituka Kanisa la Roman Katoliki wamechangia ujenzi wa kanisa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa, ametoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, azungumze na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam na Afisa Maendeleo wa wilaya ili akiwezeshe kikundi cha Sehundofe mikopo ya asilimia kumi waweze kukopa na kurejesha.
Naibu Meya Ojambi Masaburi ametumia fursa hiyo kuwapongeza kwa kupata mafanikio makubwa Sehundofe Gruop ambapo pia amesema maendeleo ni hatua hivyo aliwataka watu wawe na subira ili waweze kupata maendeleo makubwa zaidi katika Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan anayetekeleza Ilani kwa vitendo kwa kuweza kufufua fursa mbalimbali za uchumi katika nchi yetu.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari