Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online Dar es Salaam
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imetenga jumla ya Tsh. Million 36 kwa washindi 22 katika kampeni yake ya “Kapu la Wana” ambayo washindi watajishindia zawadi mbalimbali, ikiwemo gari, bodaboda, luninga na simu za mkononi.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Pilsner Lager wa SBL, Wankyo Marando, amesema Tukirudi nyuma kuangalia lengo la bidhaa hiyo, ipo kwaajili ya kusherehekea mafanikio ya walaji na kuwatunza kwa umaridadi wao kutimiza ndoto zao na kuchapa kazi.
Aidha, Kampeni hiyo itakwenda kwa muda wa miezi 8 mfululizo na itahusisha watu wote waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kushindania zawadi, baada ya kutuma nambari maalum na kupokea ujumbe mfupi wa udhibitisho.
“Pilsner Lager ni bia ya vijana ambao hawakati tamaa na wenye kiu ya kutimiza mafanikio makubwa, Tunawawezesha vijana kwa kuwapatia vitendea kazi ili wasonge mbele. Hivyo, tunawahamasisha walaji wote wa Pilsner Lager kuitumia kampeni hii ili kusogeza juhudi zao mbele.” amesema Wankyo Marando
Hivyo, ukinunua bia ya Pilsner Lager utapata kadi ya kukwangua ili kujipata zawadi kila ununuapo bia Kama zawadi ni bidhaa kama fulana, kofia tazawadiwa papo hapo Kama zawadi uliyoikwangua ni nambari maalum, itume kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 mfano: Andika Kapu 4321 Iringa (Acha nafasi), Mshiriki lazima awe na miaka 18 na kuendelea.
Kwa upande wake mshindi wa kapu la wana kwa mwaka jana Visent Kimario amesema anaishukuru kampuni ya serengeti kwa kuweza kutoa fursa mbalimbali kwa vijana hivyo wachangamkie fursa ili kubadilisha maisha.
Pia mkaguzi wa michezo ya kubahatisha Salimu amesema hii ni taasisi ya kiserikali amabayo inasimamia na kuratibu michezo ya kubahatisha ndiyo maana tupo hapa kuhakikisha tunasimamia lengo la droo ya kapu la wana.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa