December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SBL, Simba zasaini mkataba wa bilioni 1.5

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

KLABU ya Simba ambao ni mabingwa wa ngao ya jamii mwaka huu kwa kushirikiana na kampuni ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Pilsner Lager wamesaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya bilioni 1.5

Akizungumzia wakati wa utiaji saini leo Novemba 01, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries Limited, Obinna Anyalebechi amesema taasisi mbili kubwa za SBL na Simba kwa mkataba wa udhamini wa miaka mitatu, kupitia udhamini huu utaifanya bia yetu ya Pilsner Lager kuwa mdhamini wa Simba.”

“Udhamini huu utakuwa na thamani ya Tsh. 1.5 bilioni, Kwa udhamini huu tunaamini utasaidia kukuza michezo nchini kwetu. Simama Imara, Songa Mbele Kama Simba.”- Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries Limited, Obinna Anyalebechi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Simba Imani Kajula amesema Udhamini huu utasaidia uendeshaji wa klabu, gharama za uendeshaji wa vilabu huwa ni kubwa, Upatikanaji wa fedha ni muhimu sana, Tunawashukuru kukubali kuungana nasi kama wadhamini wa Simba.

“Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili, Hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka, Serengeti ni mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mwendelezo wa kusaidia mpira.”

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Bia za Serengeti Anitha Rwehumbiza amewasisitizia wanasimba kuwa wataanza kushiriki matukio ya Simba kwa kuanzia na derby na hata michezo za nje ya Dar, Kwetu ilikuwa na ndoto lakini tunafurahi tumekuja kwa muda sahihi. Tutatumia wetu, vyombo vya habari na tutakuwepo uwanjani kuitangaza Pilsner Lager na Simba.

“Tulikuwa na lengo la kupata mshirika ambaye ana mashabiki wengi, na tulikuwa na furaha tulipopata taarifa kwamba Simba ipo tayari. Ukiacha kwamba Simba na Pilsner zinaendana kwa rangi na Simba pia Nguvu Moja ya Simba ni ya kuunganisha Watanzia wote na kinywaji chao cha Pilsner Lager.”

Awali akizungumza msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Mvua ni ishara nzuri kwa Simba, Tukiwa katika wiki hii yenye thamani kubwa ya Kariakoo Dabi tumewaletea tukio lingine kubwa la kihistoria kati ya Simba na Serengeti.