November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SATA : Bado kuna upungufu wa wataalamu wa dawa za usingizi

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

CHAMA Cha Wanataaluma watoa dawa za usingizi na ngazi Tanzania (SATA) kimesema licha ya Serikali kuweka miundombinu ya kutosha katika sekta hiyo bado kuna chagamoto ya upungufu wa wataalamu wa dawa za usingizi.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam mapema leo Aprili 9, 2024, na Rais wa SATA, Dkt Edwin Lugazia wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa nane wa Chama hicho ambao ufanyika kila mwaka .

“Serikali ya awamu ya sita
imeweka miundombinu ya kutosha ya usingizi salama ikiwemo mashine za kutosha pamoja na vitendea kazi pamoja na madawa ya kutosha lakini bado tunakabiliwa na chagamoto ya kutokuwa na watoa huduma wenye weledi wa kutosha”amesema

Amesema katika kukabilina na chagamoto hiyo wamekuwa wakiendelea kujengeana uwezo katika aina tofauti za upasuaji ikiwa ni pamoja na namna ya kutoa usingizi salama pamoja na kuwahudumia mahututi ambao wanaohitaji dawa za usingizi .

“Kwa Sasa Vituo vingi vimeongezwa tunahitaji kukimbizana kufundisha watoa huduma ambao wataweza kutoa huduma hizi kila Mahali .

Aidha amesema kupitia mkutano huo ambao unafanyika kwa siku mbili na umejumuisha washiriki 250 wataweza kujadiliana na kupata mafunzo ya vitendo kwa nadharia na kubadilisha mawazo.

“Mkutano huu umekuwa ulifanyika kila mwaka kwa Wanataaluma kwa lengo la kujadiliana na kubadilisha uzoefu sambamba na mafunzo tofauti tofauti pamoja na kujengeana uwezo katika ngazi ya chini mpaka ya juu hadi ya kimataifa”, amesema

Pia amesema kupitia mkutano huo watajadiliana chagamoto wanazokubana nazo pamoja na zile zinazokabili Taifa katika huduma za kutoa dawa za usingizi na wagonjwa mahututi na kutafuta mbinu mbandala za kukabilina na chagamoto hizo.

Kwa upande wake Katibu wa SATA, Dkt John Kweyamba amesema madaktari bingwa ambao wamekuwa wakiingia katika Chama hicho wamekuwa wakipata fursa mbalimbali zilizolenga kuwajengea zaidi .

“Wataalamu hawa wanapojiunga na Chama chetu wamekuwa wakipata fursa ya kwenda kujiendeleza katika nchi mbalimbali ambazo wanamahusiano nazo kana Chama na kuiwezesha nchi kupata wataalamu wabobezi zaidi.

Hata hivyo amesema licha kuwepo Kwa chagamoto Chama hicho kimekuwa kikizifanyia kazi .

“Tunakili kuwa chagamoto zipo lakini Kwa sasa zimepungua kutokana na madaktari bingwa nchini kuongezeka..
tumekuwa tukiwajengea uwezo katika mikoa hasa waunguzi Kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi”amesema

Aidha amesema Chama hicho kimekuwa kikishirikiana na Serikali katika kupunguza chagamoto hizo.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wataalamu kuzidi kuungana kwa pamoja ili kujenga Taifa lenye wataalamu bora na kutengeneza afya bora kwa wananchi.