Na Hadija Bagasha,TimesMajira Online,Tanga
“NIMEKUJA hapa (Tanga) niwasalimie, lakini kubwa niwape salamu za Rais, Rais anawasalimia sana na anawashukuru sana kwa kazi nzuri mliyofanya mwaka jana kurudisha Serikali ya CCM madarakani, Rais anasema tupo salama, tuchape kazi, twende vizuri,tujenge upendo na mshikamano wa Watanzania ili Taifa letu likuwe, liwe na tija zaidi;
Hayo yamesemwa jana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan baada ya kuanza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi kwenye jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Pia amewataka Watanzania kuacha kusikiliza maneno yanayozua taharuki na kuvuruga mshikamano na badala yake washirikiane ili kudumisha amani ya nchi iliyopo.
Makamu wa Rais amesema kwa sasa kumeibuka maneno mengi ambayo asilimia kubwa yanatoka nje hivyo aliwahakikishia Watanzania kuwa wako salama kubwa zaidi waendelee kushikamana na kudumisha amani ya nchi iliyopo.
“Kama mnavyojua hivi sasa maneno ni mengi, ni mengi mno nataka kuwahakikishia kwamba mpo salama, hivyo Watanzania tushikamane, tushirikiane wote tusimame kama watanzania kuijenga nchi yetu,”amesistiza Makamu wa Rais.
Ameongeza kuwa, maneno hayo mengi mengine hayatoki ndani yanatoka nje, “hivyo wapuuzeni endeleeni kufanya dua zenu, lakini tushirikiane, tushikamane, twende na Tanzania yetu tupo salama,”alisema.
Aidha, mama Samia amesema madhumuni makubwa ya kufanya ziara mkoani Tanga ni kupita na kuangalia, shughuli za maendeleo zinazoendelea hasa katika majengo ya utawala, miradi ya maji, afya na miradi mingine inayotekelezwa na kujua namna ya kutatua changamoto ili miradi iweze kuendelea.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba