Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SERIKALI imesema ukamataji mkubwa ambao haukuwahi kutokea katika historia ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka jana umetokana na dhamira ya dhati na utashi wa kisiasa wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesemwa Bungeni jana na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, wakati akiwasilisha Bungeni taarifa ya hali za kulevya nchini.
Amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2023 umekuwa wa kipekee sana katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kwani wamefanikiwa
kukamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kuliko wakati
mwingine wowote katika historia ya mapambano ya dawa za
kulevya hapa nchini.
Amesema dawa za kulevya zilizokamatwa ni kama ifuatavyo; Heroin
Kilogramu 1,314.28, Cocaine kilogramu 3.04, Methamphetamine
Kilogramu 2,410.82, Bangi Kilogramu 1,758,453.58, Mirungi
Kilogramu 202,737.51 na Skanka Kilogramu 423.54.
Kwa upande wa na Dawa Tiba zenye asili ya kulevya zilizokamatwa ni gramu 1,956.9 na mililita 61,672.
Aidha, Waziri Mhagama, amesema kiasi hicho cha dawa za kulevya kilogramu1,965,340.52 kilikamatwa katika kipindi cha Januari – Desemba 2023.
“Kiasi hiki ni karibu mara tatu ya kiasi cha dawa za kulevya zilizokamatwa nchini kuanzia mwaka 2012 hadi 2022, ambacho ni kilogramu 660,465.4,” amesema Waziri Mhagama.
Amesema Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ilifanikisha ukamataji wa jumla ya kilogramu 1,965,340.52 zikihusisha watuhumiwa 10,522 (wanaume 9,701 na wanawake 821).
Aidha, amesema dawa ngeni zilizoanza kuingizwa nchini hivi karibuni kama vile methamphetamine, skanka na biskuti zilizochanganywa na bangi pia zilikamatwa katika kipindi hicho.
Katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya
yanaimarishwa nchini, alisema Serikali imenunu Boti yenye mwendo kasi (Speed Boat) ambayo pamoja na shughuli zingine itakuwa ikifanya doria baharini ili kufuatilia vyombo vinavyohisiwa kuingiza dawa za kulevya nchini kama vile Heroini, Methamphetamine na nyingine.
Aidha, amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za tiba kwa watu wenye uraibu wa dawa za kulevya ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo.
Amesema hadi Desemba 2023, Serikali ilikuwa na vituo 16 vya tiba saidizi na unasihi kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT Clinics). Vituo hivi viliwahudumia waraibu wa dawa za kulevya 15,912.
Aidha, Katika kipindi hicho kulikuwa na nyumba 56 za upataji nafuu (sober houses) zikihudumia waraibu 3,488. Serikali ilisimamia kikamilifu uanzishaji na Uendeshaji wa nyumba hizi.
Hata hivyo, amesema pamoja na mafanikio hayo bado tuna safari ndefu katika kupambana na janga hili, kwani ni wazi kuwa bado dawa za kulevya zinaingia nchini kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji katika nchi zinazozalisha dawa hizi, kubadilika kwa teknologia za
uzalishaji na usafirishaji pamoja na utandawazi. Â
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika