Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan amempigia simu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na kutaka kujua hali inayoendelea katika uzinduzi wa kambi ya madaktari bingwa na wabobezi mkoani humo.
Akizungumza kupitia simu, Rais Samia amemuhakikishia RC Makonda kuwa ataongeza nguvu kubwa katika kambi hiyo kwa masilahi mapana ya kuendelea kutolewa kwa huduma bora kwa wananchi wa Arusha.
Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa wananchi wa Arusha kutumia fursa hiyo vizuri kwa kujitokeza kwa wingi kwenye ushiriki wa kupata huduma hizo za afya.
Aidha, Rais Samia ametoa pongezi kubwa kwa Hospitali zote, taasisi za afya na mashirika yote ambayo kwa pamoja wamekubali kushirikiana na RC Makonda katika kutoa huduma bure kwa wananchi kwa siku zote 7 kuanzia Julai 24 hadi 30, 2024.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani