December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia aendelea  kukoleza dhamira yake akiwa Rukwa

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Rukwa

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kuyapeleka katika Mikoa ya Rukwa, Katavi hadi Singinda katika kutekeleza mkakati wa kumtua ndoo Mama  kichwani.

Ametoa kauli hiyo jana wilayani Nkasi baada ya kupata vilio vya wabunge wa Nkasi kwenye mkutano wa hadhara.

 Wabunge Vicent Mbogo  wa Nkasi Kusini na Aida Khenan wa Nkasi Kaskazini walimweleza Rais Samia kuwa licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kutatua tatizo la maji Nkasi, lakini suluhisho la kudumu la maji na kutoa maji Ziwa Tanganyika.

Amesema kwa sasa Serikali ipo katika hatua za awali za kuyatoa maji Ziwa Tanganyika na kuyapeleka Singida na  ameziagiza Wizara mbili ya Maji na ya Kilimo kuanza mchakato huo.

Amefafanua kwamba  wapo katika hatua ya kumpata  Mhandisi mshauri na kuwa lengo la Serikali ni kutaka kuona tatizo hilo la maji linakwisha  kwa kuweka mradi wa uhakika na wa kudumu.

Sambamba na hilo , amesema  amezindua Hospitali ya Wilaya Nkasi ambayo imejengwa kwa thamani ya sh. Bil.8 na kufurahishwa na utekelezwaji mzuri wa ujenzi wa hospitali hiyo na kuwa lengo la Serikali ni kutaka kuimarisha sekta ya afya Ili kuwe na watu wenye afya wanaoweza kutoa mchango kwa taifa.

Hivyo amewataka wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya na kuwa mwelekeo wa sasa ni kutaka kuona huduma za afya zinatolewa kwa bima na kuwa jambo hilo limejadiliwa bungeni na kupitishwa kama sheria na kuwa sasa ni wakati wa jamii nzima kujipanga na bima.

Amesema  bima ya afya ni uhakikisho wa afya ,kwani kila mmoja anakuwa na uhakika wa afya kwa kupata huduma bora na zinazotakiwa kulingana na maradhi anayougua mgonjwa na kwamba  suala hilo la muhimu sana katika kipindi hikii.

Wakati huo huo,  Rais Samia amekataa daraja kupewa jina lake na kupendekeza heshima hiyo apewe Mama Maria Nyerere kutambua mchango wake kwa Baba wa Taifa katika  kupambania Uhuru.

Rais  Samia  ameendelea na ziara ya kikazi ndani ya mkoa wa Rukwa jana  kwa kuzindua Miradi mbalimbali ya maendeleo na kupokelewa kwa kishindo na wakazi wa Sumbawanga.

Awali Rais Samia alizindua jengo la ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kalambo ambalo limegharimu  zaidi ya sh. billion 5  kisha kufuatiwa na uzinduzi wa Barabara  ya Sumbawanga-Matai-Katanga yenye urefu wa kilometa 107.14 anabyoimegharimu jumla ya sh. bilioni 105.

 Barabara hiyo itasaidia kurahisisha usafiri na uchukuzi ambapo hapo awali ilitumika siku nzima wananchi kusafiri kupata huduma maeneo yanayounganishwa na barabara hiyo.

Rais Samia pia alipata wasa wa kuzungumza  na maelfu ya wakazi wa kalambo waliojitokeza kumlaki  katika ziara hiyo alipokuwa anafungua barabara hiyo ya Sumbawanga, Matai na Ksanga na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kufanya jitihada kuhakikisha huduma muhimu zinaboreshwa kwa ajili ya ustawi wa jamii nzima.

Vilevile Rais Samia amezindua Vihenge , maghala ya kuhifadhi chakula ya NFRA na msimu wa ununuzi wa nafaka eneo la konondo Halmashauri ya Sumawanga.

 Mradi huo umegharimu jumla ya sh. billionaire 14 katika hafla hiyo Rais Samia amewasihi wananchi kuchangamkia fursa za kuzalisha kwa wingii mazao yapate masoko nje ya nchi kupitia NFRA.