December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sakata la Bandari, Wabunge wa Ilala wafunguka

Na Heri Shaaban (Ilala )Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala wamesema sakata la madai ya kuuzwa Bandari ya Tanzania ni matango poli kwa ajili ya vita ya kiuchumi.

Wabunge wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala walitoa tamko hilo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Spika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,alisema suala suala la Bandari ya Tanzania ni makubaliano ya kimataifa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesaini mkataba tuu ,Bandari haijauzwa .

“Suala la Bandari ni sawa na matango poli yasio liwa wivu wa vita ya kiuchumi hili ni kundi la watu wanataka kutugawa na Serikali yetu hivyo watanzania naombe muwapuuze ni kundi la watu wachache wanaeneza habari hizi “alisema Mbunge Zungu .

Mbunge Zungu alisema Watanzania wote wapo salama,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yupo salama ndiye mgombea uras wa mwaka 2025 atakayeshinda kwa kishindo hivyo msigawanyike .

Aidha alisema sasa hivi tunaelekea katika Uchaguzi wa kushika dola Serikali za Mitaa Mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 hivyo waje tuwapige CCM itaibuka na ushindi mnono katika chaguzi zake zote.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa alisema suala la Bandari SERIKALI yetu ipo macho aijalala inasimamia kuakikisha inafanya kazi kwa siku moja kupakua mizigo ya abiria.

Aidha Mbunge Jerry Silaa alisema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina viongozi makini wakiongozwa na Mwanasheria Makini Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Turia na Naibu Spika Mussa Zungu kilichofanyika Bandari ya Dar es Salaam makubaliano ya Tanzania na Dubai kwa ajili ya kuwekeza ni mkataba lwa ajili ya kuboresha Bandari .

Alisema makubaliano hayo ni nchi kwa nchi na serikali kuna kundi la watu wanadai Bandari imeuzwa sio taarifa sahihi watanzania zipuuzeni kablasha amepitia lote watu wanaopinga wamekosa uelewa wasio itakia mema Tanzania .

Mbunge wa Jimbo la segerea Bonah Ladslaus Kamoli, alisema Bandari ya Tanzania aijauzwa ni makubaliano ya kufanya biashara kama ni mchumba ametolewa posa ya mahali .

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar wa Salaam Abbas Mtemvu ,aliwataka Wananchi wa Jimbo la Segerea,Jimbo la Ukonga ,na Jimbo la Ilala wote wenye kero kuwasilisha Ofisi ya Mbunge kwa ajili ya Utatuzi wake kutatua kero za Wananchi.