October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Saa 48 zimebaki wagombea uchaguzi mkuu kunadi sera

Na David John, TimesMajira Online

IKIWA imebaki siku mbili kuingia katika uchaguzi mkuu wa Rais ,Ubunge na Udiwani joto linazidi kupanda ambapo wagombea mbalimbali wameendelea kumwaga sera zao kwa wananchi kwa lengo la kutafuta turufu ya kuchaguliwa na wananchi.

Wagombea ambao wapo katika siku za lala salama huku kila mtu amekuwa akitumia mbinu mbalimbali ambazo hazipingani na kanuni , Sheria na taratibu za tume ya Taifa ya uchaguzi ili kuhakikisha anashinda.

Hivi sasa pilika pilika za wagombea wakionekana kumwaga sera huku kila mmoja akivutia upande wake kwamba endapo atachaguliwa atahakikisha anafanya kazi kwa karibu na wananchi na kuondoa kero ambazo zimekuwa sugu kwenye maeneo yao.

Mgombea udiwani Kata ya Tungi Kigamboni wilayani humo Jijini Dar es Salaam Ally Sharifu amesema, ameamua kugombea udiwani katika kata hiyo kutokana na changamoto ambazo wanakabiliana nazo wananchi wake.

Amesema, kata hiyo kwa vipindi tofauti imeongozwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi lakini kwa bahati mbaya wameshindwa kukidhi matakwa ya wananchi katika kutatua kero zilizopo ndani ya kata hiyo.

Sharifu amesema, ni wakati Sasa kwa wananchi wa kata hiyo kufanya maamuzi na kuchagua Mgombea wa udiwani kupitia Chama Cha Act _Wazalendo ambacho kimejipambanua kwa kutaka kuwaletea Maendeleo ya kweli

Amesema, Kata ya Tungi kwa miaka Mingi imekuwa kama yatima kutokana na viongozi wanaochaguliwa kushindwa kuwatumikia wananchi wa kata hiyo, kutokana na mwitikio wa wananchi kuwa mkubwa kwenye makutano yake anaamini Chama chake kitashinda.

“Kimsingi tunaomba tu uchaguzi uwe wa Uhuru na haki na wakishindwa basi washindwe kwa haki na wao watakuwa tayari kukubali lakini pakiwepo hila hawatakubali kirahisi,” amesema Sharrifu mgombea wa udiwani kupitia Act _ Wazalendo.

Sharifu amesema, wananchi wa tungi hadi Sasa wameonyesha kutaka mabadiliko na kuunga mkono kauli mbiu ya kazi na bata ambayo unapatikana katika chama Cha Act Wazalendo nahakuna shaka kwamba watamchagua kuwa Diwani wao.

Amesema, moja ya kero na changamoto kubwa ambazo zimewachosha wananchi wa kata ya Tungi ni pamoja na mafuriko ambapo nyakati za mvua wananchi wa kata hiyo wanashindwa kabisa kufanya shughuli zao kutokana na mafuriko ya maji.

Mgombea huyo amesema, licha ya uwepo wa mafuriko mara zote viongozi wanaopewa dhamana wameshindwa kutafuta njia mbadala kuhakikisha maji hayo yanakwenda katika Bahari ya Hindi badala yake wananchi wanakuwa kama wapo kisiwani, hivyo endapo wananchi watafanya maamuzi na kumchagua yeye atahakikisha anashughulikia kero hiyo.

“Nataka niwahakikishie wananchi wa kata ya Tungi, endapo watanichagua nitahakikisha mafuriko Tungi basi kwani tutashirikiana kwa pamoja ili miuondombinu inajengwa na maji yanaelekezwa Baharini,” amesema Sharifu.

Sharifu ameongeza, watashirikiana pamoja kujenga miundombinu ya mifereji na mitalo ili kuelekezea maji kwenda bahar,i hivyo ili hayo yatekelezeke anawaomba wananchi wa Tungi kuchagua Act Wazalendo na kumchagua yeye kuwa mtumishi wao.

Amesema, kitu kikubwa ni kila mwana Tungi kuhakikisha anatuza kadi yake ya Mpiga kura na siku ikifika kwa maana oktoba 28 kwenye sandugu la kura wanamchagua yeye kuwa Diwani wao.

      Kuhusu usalama ndani ya kata hiyo 

Sharifu Amesema, awali wakati akiwa mjumbe kwenye kata hiyo alijitajidi kuhakikisha kata na mitaa yake inakuwa salama lakini baada yeye kutoka hali ya usalama ilikuwa hafifu, hivyo endapo watamchagua atahakikisha mitaa yote ndani ya kata ya Tungi inakuwa salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao kwa Nyakati zote.

Amesema, amejipanga vyema kuhakikisha kata ya Tungi na viunga vyake inarudi katika hali ya usalama Kama ilivyokuwa huko nyuma na mara baada ya kuingia madaraka kupitia Ofisi yake ya kata ataratibu vijana ili kuweza kuazisha vikundi vya ulinzi shirikishi kwa lengo la kuhakikisha usalama unaimarika kwa kushirikiana na Jeshi la polidi

Lakini pia kuona uwezekano wa kuongeza vituo vya polisi ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu zaidi ukizingatia Kuna vituo vichache na kata hiyo ni kubwa.

Kuhusu wavuvi, Sharifu amesema kama inavyofahamika kuwa Kigamboni ni moja ya eneo ambalo linapatikana wavuvi atahakikisha wanapata haki zao kwani pamekuwepo na kero za kukamatwa mara kwa mara na kuzuiliwa kuvua kwa sababu ambazo wakati mwingine hazieleweki kisheria.

Sharifu anafafanua na kuwataka wavuvi waweze kumuunga mkono kwani wakifanya hivyo changamoto zao zinakwenda kutatuliwa kwa asiliamia mia moja.

Amesema, anatambua kuwa wavuvi wanakabiliwa na kero ya tozo za leseni kinyume na sheria na taratibu za uvuvi suluhu ya hilo ni kumpa kura za ndio oktoba 28 mwaka huu, ili aweze kuingia madarakani mwisho kushughulikia changamoto zao.

Kuhusu mikopo kwa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu amesema, wakimpa nafasi hiyo ya udiwani kupitia vikao vya Baraza la madiwani atahakikisha anapambania haki hiyo ili makundi hayo kuweza kupata mikopo.

“Kuna fedha pale Halmashauri kwa ajili ya makundi haya lakini hivi Sasa fedha hizi zinapatikana kwa kujuana au kwa kuangalia ukada wa vyama, nataka niwaambie wananchi wangu wa Tungi mimi nitakuwa Diwani adiyeangalia mtu katika chama gani bali nitatenda haki sawa,”amesema.

Hata hivyo amesema, anajua wapi fedha hizo zinapotelea hivyo jambo kubwa ni kumpa Kura za ndio atahakikisha wananchi wa Kigamboni hususani kata ya Tungi wanapata mikopo tena pasipokuwa na liba Kama serikali kuu ilivyoelekeza.

Kupitia fedha za TASAF kwa kaya masikini, Sharifu amesema atahakikisha wanaostahili ndio wanaofaidika na fedha hizo tofauti na ilivyo sasa ambapo watu ambao wanaostahili hawapati na wasiostahili ndio wanaipata jambo ambalo si sawa.

“Mimi Ally Sharif ndio tumaini pekee la wananchi wa Tungi nawaomba msifanye makosa Kama mnavyofanya huko nyuma chagueni Act _wazalendo. kauli mbiu yetu kazi na bata, kwa maana rasilimali za taifa letu lazima ziwe kwa faida ya watanzania wenyewe,”amesema Sharifu.

Kuhusu ajira kwa vijana

Mgombea huyo wa udiwani kwa tiketi ya Act Wazalendo amesema, amejipanga vizuri kuhakikisha nafasi zote za ajira zinapopitia kwenye Ofisi ya kata chini ya uongozi wake basi hakutakuwa na ubaguzi wowote kwani atakuwa mstari wa mbele kuona vijana hususani kata yake wanafaidika na nafasi hizo.

Amesema, anajua kuna nafasi mbalimbali za ajira zinakuja kupitia Ofisi ya mtendaji kata lakini pamekuwepo na kuangalia sura ya mtu nakujuana, hivyo chini ya uongozi wake kila kitu kutakuwa sawa na haki itatendeka kikubwa wananchi wakubali mabadiliko.

“Nawaomba wananchi wezangu wenyewe ni mashahidi chini ya Chama Cha Mapinduzi hakuna kilichofanyika, nichagueni Mimi Ally Sharif kuwa Diwani wa kata ya Tungi, nitasimamia suala zima la elimu, afya na maeneo mengine,”amesema Sharifu.

Uchaguzi Mkuu utarajia kufanyika kesho kutwa Oktoba 28, ambapo wananchi watapata fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka ili wawatumikie katika kipindi kingine cha miaka mitano.

%%%%%%%%%%%%%%%%