Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
YUSTAS Rwamugira amekuwa mgombea wa tisa kuchukua fomu katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)akiwa na Mgombea mwenza Amana Suleiman Mzee kutoka Chama cha Tanzania Labour Party(TLP).
Wagombea hao wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele huku wakitaja vipaumbele vitatu ambavyo ni Ulinzi na Usalama wa Nchi,Utawala Bora na Uchumi imara.
“Kwanza nchi ili itawalike lazima iwe salama na ikae imara na kila mmoja ahakikishe tupo salama na katika uchaguzi huu tutaufanya kwa amani,kazi zetu tutazifanya kwa amani,utulivu na usalama wa nchi,”amesema.
Amesema kama nchi Lazima iwe na utawala bora ili kila kitu kiende kwa utaratibu kwa mujibu wa katiba ya nchi,sheria za nchi zilindwe na huo utawala bora ndiyo utakaotufanya nchi kufanya kazi vizuri ili kujenga uchumi wa nchi na tunataka uchumi imara.
“Sasa hivi tunavijana wengi wamemaliza shule hawana kazi,hivyo lazima tuhakikishe hawa vijana,serikali ya TLP inatengeneza mazingira mazuri ya uchumi ambao ndiyo utatusaidia kazi za kufanya.
“Na kazi zipo,tuna ardhi kubwa tuna watu zaidi ya mil.60,tuna madini,tuna mashamba,tunamabahari,tunamifugo ya kila aina mifugo,mbuzi,kuku kwahiyo lazima vile tuvitengeneze viwe katika utaratibu vizuri,”amesema.
Amesema Chama ndani ya miaka mitano kitasimamia mambo hayo yakae vizuri na wanataka vijana wote shuleni wajifunze ufundi kuanzia shule ya msingi,chekechea mpaka Chuo kikuu.











More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako