December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ruvu Shooting ‘yakata’ watano

Na Mwandhishi Wetu, TimesMajira Online

UONGOZI wa klabu ya Ruvu Shooting umetangaza kuachana na nyota wao watano kuelekea msimu mpya waLigi Kuu Tanzania Bara (VPL) 2020/2021utakaoanza kutimua vumbi rasmi Septemba 6.

Nyota hao waliotemwa ni Rajab Zahir, Jamal Mnyate, Salum Makota Edward Christopher na Adam Faraja ambao nafasi zao zitachukuliwa na wachezaji wengine watano wanaocheza wanaocheza nafasi ya beki wa kushoto,beki wa kulia na kati pamoja na washambuliaji wawili.

Afisa habari wa klabu hiyo Massau Bwire amesema kuwa, maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya kikao maalum kilichofanyika leo asubuhi kilichotumika kusajili taarifa ya benchi la ufundi linaloongozwa na Salum Mayanga ambaye pia ametoa ushauri nini kifanyike kwa ajili ya mafanikio zaidi ya msimu ujao.

“Katika ripoti iliyotolewa benchi la ufundi limependekeza majina ya wachezaji wapya ambao tutawataja baada ya kumaliza nao mazungumzo na kusaini na tunaamini endapo tutawapata basi itakuwa ni faraja kwa timu yetu, ” amesema Masau Bwire.

Aidha amesema kuwa, wao kama klabu wataendelea kuwaachia masuala ya usajili na ufundi kwa benchi la ufundi ambao ndio wanatambua uzuri na ubora wa wachezaji wanaowafaa.