Na Esther Macha,TimesMajira Online, Mbarali
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya imekabidhi Trekta za mikono saba ,Pikipiki tano na Guta moja kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2020/2021 ambavyo vimetokana na asimilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Akikabidhi mikopo hiyo kwenye ofisi za Halmashauri hiyo, Mwenyekeiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Twalib Lubandamo amesema kwamba mikopo hiyo yenye thamani ya Sh. milion .99 imetolewa kwa vikundi vilivyokidhi vigezo ili kuweza kuviwezesha kujishughulisha na uzalishaji mali hususan kilimo .
Aidha Lubandamo amesema kuwa historia ya ulejeshaji wa mikopo kwa wilaya ya Mbarali upo chini Halmashauri imeandaa mkakati wa kuvifuatilia vikundi vyote vilivyonufaika na mikopo hiyo ili vikundi vingine viweze kunufaika.
“Katika Halmashauri yetu vikundi vilikuwa ni vingi vilivyoomba mikopo, tumeanza na ninyi kutokana na fedha tulizokuwa nazo, tumewapa mikopo hii mkiwa mnafurahi, tunaomba sasa mmalize mkiwa mnafurahi ili msije baadae mkanuna,” amesema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri.
Hata hivyo Lubandamo amesema kwamba mikopo hiyo inatolewa kama bure kwani haina riba hata moja na kwa sababu mmeshikliia fedha za vikundi vingine tunawaomba ule muda ambao tumekubaliana mikopo hiyo irejeshwe kwa wakati ili na vikundi vingine viweze kunufaika kama mlivyonufaika.
Akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo ,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Daniel Kamwela amesema kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020-2021 kiasi cha million 212 ambazo ni asilimia 10% ya mapato ya ndani kwa kipindi cha Julai hadi Desemaba ziliweza kutolewa kwa vikundi vya wanawawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa asilimia 100%
Aidha Kamwela amesema kuwa, fedha hizo zimegawanywa kwa vikundi vitano vya wanawake vyenye wanufaika 91, vikundi 10 vya vijana vyenye wanufaika 132 pamoja na vikundi 4 vya watu wenye ulemavu vyenye wanufaika 24.
Christus Mwageni ni Afisa vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali amesema kuwa kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2020/2021 Halmashauri imefanikiwa kutoa kiasi cha shilling milioni 99,500,000 ambapo fedha hizo zote zimetumika kununulia Trekta za mikono mbili ambazo zimetolewa kwa vikundi vya wanawake, Trekta tano za mkono, Pikipiki tano pamoja na Guta moja ambavyo vyote vimetolewa kwa vikundi vya Vijana vitano.
Mwageni ameongeza kuwa, zoezi la utoaji wa vifaa kazi umekuwa ni bora zaidi kwani unaleta ufanisi kwenye vikundi, vilevile eneo la Mbarali ni eneo la kilimo, vifaa hivyo vitawawezeza kufanya shughuli zao badala ya kushinda vijiweni na wameamua kutoa vifaa sababu baadhi ya vikundi vikipewa pesa vinakwenda kugawana badala ya kutimiza malengo waliyojiwekea.
Wakiongea kwa niaba ya wenzao Seif Mohamendi na Asia Shaibu wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha vitendea kazi hivyo na wameahidi kuvitumia vizuri vifaa walivyokabidhia ili waweze kurejesha fedha walizokopa kwa muda uliopangwa ili vikundi vingine viweze kunufaika.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu