Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limewataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya kuto jihusisha na vitendo vya ushoga na uvutaji bangi ambavyo vinaweza kuathiri suala zima la elimu yao kutokana na kuchelewa kupata mkopo.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga wakati akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioripoti chuoni hapo kwa ajili ya kuanza masomo yao.
“Kuna tatizo hili katika jamii (ushoga)la kujamiana watu wa jinsia moja hasa wanaume naomba sana kwa nyie wanaume msijekuwa mnaenda kujiuza sababu bumu limechelewa ili muweze kupata fedha na kununua mahitaji hili suala lipo hata hapa Mbeya nyie mtaona tu utaona wanaume wanakusogezea chips mayai na nyumbani ulizoea viazi tu ukila malipo yake utayaona baada ya muda vitu hivyo havijifichi unaanza kutembea ovyo ovyo sisi tutawagundua tu,”ameeleza Kuzaga na kuongeza kuwa
“Nyinyi wenyewe mlikuwa mnasoma mitandao ya kijamii mimi ndo mtu wa kwanza kutangaza mtu aliyekuwa amefanyiwa vitendo vya ushoga na alifungwa miaka 30 je na wale waliokuwa wanahusika,”.
Kamanda huyo amesema kuwa watu walikuwa wanaogopa kulisema hilo kuwa Tanzania hakuna ushoga lakini alitangaza hilo kuwa kuna mtu kafanya vitendo hivyo hata hapa sitaki kusikia suala la ushoga kwa nyie wageni na hapo Mafiati maeneo ya mataa kuna Bar wanauza vinywaji watu wapo wapo tu sio kwamba wanawatafuta wanadada hapana wanawatafuta akina kaka.
“Unaweza kusema wanawake wamepona lakini akina kaka wanakuwa wameshaharibiwa na kuna wengine wamekuja na vitendo hivyo toka walikotoka,nawaombeni hili lisiwepo kabisa na tukipata taarifa hizo na ikionekana kuna mtu anajihusisha na vitendo hivyo toeni taarifa polisi au uongozi wa chuo ili mwanafunzi anayejihusisha na vitendo hivyo aweze kuondolewa kwenye jamii ya chuo na nimegusia hili kuweza kulinda usalama wa afya zenu, “amesema Kamanda Kuzaga.
Kwa upande wake Mlezi wa wanafunzi wa chuo hicho , Florence Kalimbikulu ameshukuru ujio wa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya sababu elimu watakayotoa itawasaidia kwani kumekuwa na matukio ya wanafunzi kukamatwa usiku na kushindwa kufahamu nyakati hizo zwanakuwa wanafanya nini.
Aidha Kalimbikulu ametoa ombi kwa Kamanda huyo kuwa maeneo ya Msikitini mpaka Benki Kuu kunakuwa na magari ya watu wenye fedha yanapaki pande zote mbili kiasi kukosa sehemu za kupita na kusababisha wanafunzi kugongwa na magari nyakati za usiku.
“Mkuu wa chuo utanisamehe kulisema hili sababu unajua ni jinsi gani ninavyoteseka na hawa watoto kuwapeleka hospitali pindi wanapogongwa na magari nyakati za usiku sababu eneo lile hakuna sehemu ya kupaki magari,”amesema Mlezi huyo.
John Jorojick ni mwakilishi wa Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Jamii amesema kuwa ameomba kuwepo na usalama kwa wanachuo kipindi hiki ambacho chuo kimefunguliwa na kwani wezi wanaongezeka mtaani na kuomba doria kuongezwa ili wanafunzi waweze kuwa salama na mali zao.
More Stories
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini
Tanzania mwenyeji mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika