December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Royal Tour kuja kivingine Dodoma.

Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Philip Mpango kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa filamu ya Royal tour jiiini Dodoma baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua filamu hiyo nchini Marekani na maeneo mengine nchini.

Hatua hii imekuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Anthony Mtaka kutumia siku ya wafanyakazi -Mei Mosi kuomba kibali cha Rais Samia ili filamu hiyo izunduliwe mkoani hapa na kutoa fursa mbalimbali za utalii na kubainisha fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma pamoja nakuhamasisha utalii wa makao makuu ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameeleza kuwa uzinduzi wa filamu hiyo utafanyika  siku ya jumapili tarehe 15/05/2022 kuanzia saa 12:00 Jioni  katika Ukumbi wa mikutano wa JK Conversion Center.

Amefafanua kuwa  uzinduzi huo utahusisha matukio mbalimbali ikiwemo maonyesho ya utamaduni wa asili ya wenyeji wa mkoa wa Dodoma,mazao ya zabibu na ngoma za kitamaduni za kigogo na kirangi.

“Maandalizi yamekamilika kutakuwa jogging na burudani itayobebwa na utamaduni  wa Dodoma ngonga za kigogo na kirangi,milango iko wazi kwa watakaopenda kujiunga na tukio hili,”amesema

Mtaka ametumia nafasi hiyo kuzitaka sekta binafsi,wafanyabiashara na Wadau wa maendeleo  kushiriki kwenye tuki hilo ili kukuza sekta ya utaalii na kufungua mipango ya sekta ya uchumi

“Zao la zabibu linaongeza thamana ya yake kutoka kwenye wine kwenye mvinyo, tutakuwa na maonyesho ya mazao ya zabibu pia,”amesema

Amesema kuwa Ofisi yake imetoa fursa kwa baadhi ya Wilaya kuangalia tukio hili kupitia vyombo vya habari na utaratibu wote umekamilika.

Ikumbukwe kuwa mbali na Dodoma filamu ya Royal Tour  ilianza kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko nchini Marekani na hatimae jijini Arusha ,Zanzibar  na Dar es Salaam.