January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rosa Ree afunguka Mwanaume anayemtaka

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII anayefanya vizuri katika muziki wa Rap hapa nchini Rosa Ree, amefunguka na kuweka wazi kuwa baadhi ya vigezo anavyovitaka kwa mwanaume wake atakayemuoa, moja ya ndoto zake kubwa ni kuja kuwa mama na mwanamke mzuri kwa mwanaume ambaye Mungu amempangia.

Akiweka wazi hilo kupitia shoo ya Friday Night Live ya East Africa TV na East Africa Rosa Ree amesema anapenda kuwa na mwanaume ‘smart’, anaejielewa, kumcha Mungu pia awe na akili.

“Moja ya ndoto zangu kubwa ni kuja kuwa mama na mke mzuri kwa mwanaume ambaye Mungu atanipangia, ambaye atakuwa smart, anayejielewa, mwenye akili na mcha Mungu,” amesema Rosa Ree.

Hata hivyo Rosa Ree amesema, ili kumpata mume wa aina hiyo inabidi mwenyewe ujielewe, huwezi kuwa wa aina fulani halafu ukampata mtu tofauti. Jinsi mtu utakavyojiweka ndiyo utapata mwanaume wa aina hiyo.