Ronaldo akutwa na Corona
RISBON, Uremo
MSHAMBULIAJI wa Juventus na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona na ameacha kwenye kikosi cha timu ya taifa ili kujitenga na wenzake.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 35, alianza michezo yote miwili ya Ureno wiki iliyopita na sasa atakosa mchezo wao wa pili wa Kombe la Mataifa Ulaya dhidi ya Sweden mchezo utakaochezwa leo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Chama Cha Soka Ureno kimesema, Ronaldo aliachwa kufanya mazoezi na timu ya taifa baada ya kupimwa virusi vya Corona na kukutwa navyo hivyo hatoshiriki katika mchezo wa leo dhidi ya Sweden.
Hata hivyo Ronaldo, alianza kampeni ya 2020/21 kwa kiwango cha hali ya juu baada ya kufunga goli katika ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Sampdoria kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Italia chini ya kocha Andrea Pirlo.
Ronaldo amekuwa mchezaji wa 30 katika Ligi Kuu Italia Serie A aliyeambukizwa virusi vya Corona wengine walikuwa, Roberto Gagliardini, Radja Nainggolan, Milan Skriniar na Alessandro Bastoni.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM