Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wameandaa kikao na wadau kitakachofanyika Jumatatu tarehe 18, 07, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika kikao hicho anatarajiwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Julai 14, 2022 Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bi. Angela Anatory amesema kuwa Lengo kuu la kikao ni kuzungumza na wadau kuhusu mwelekeo wa RITA ilipotoka, ilipo na inapoelekea pamoja na kupokea maoni, ushauri, na nini kifanyike katika utoaji wa huduma ambazo RITA wanazitoa kwa Wananchi kwa ustawi wa Jamii na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
“Tumealika Taasisi za Dini, wizara mbalimbali, taasisi mbalimbali za serikali, wadau ambao ni balozi za nchi zinazowakilishwa katika nchi yetu Tunatarajia kuzungumzia mafanikio tuliyoyapata, changamoto zinazotukabili na namna tulivyojipanga kukabiliana navyo na mikakati tuliyojiwekea katika kukabiliana na changamoto hizo” Amesema Angela
Mbali na hayo, Angela aliyataja mafanikio ambayo kama Taasisi wameyapata katika eneo la utoaji huduma ambapo wamefanikiwa kubuni programu mbalimbali za usajili zilizoleta matokeo makubwa;
“Wakala kama taasisi ambayo inajishughulisha na masuala ya usajili tumeweza kubuni programu mbalimbali za usajili ambazo zimekuwa na matokeo makubwa sana programu ambayo imekuwa na matokeo makubwa ambayo tulianzisha mwaka 2013 tulishirikiana na wadau wa maendeleo tunaiita ni programu ya usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano”
Angela amesema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya mwaka 2012 ni kwamba kiwango cha chini cha watoto ambao walisajiliwa na kupata vyeti wa kundi hilo ni 13% na mpaka sasa kwa takwimu zao za ndani wameweza kuongeza kiwango cha usajili kutoka 13% mpaka sasa wapo kwenye 65% ambayo ni sawa na usajili wa watoto zaidi ya milioni 7.7
Angela amesema changamoto waliyokutana nayo katika usajili wa watoto hao wenye umri wa chini ya miaka 5 ni kusogeza usajili kutoka kwenye ngazi ya Wilaya na kuupeleka kwenye ngazi ya halmashauri kwa maana ya kwamba wanasajili kwenye vituo vya tiba ambavyo vituo hivyo vinatoa huduma ya Afya ya uzazi lakini pia wanasajili kwenye kata
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito