Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ametoa wito kwa vijana kuchagamkia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mikopo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Kikwete ametoa wito huo alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu lilipo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa sabasaba .
“Serikali imeendelea kutenga fedha kuhakikisha makundi mbalimbali yananufaika kwa mfano kupitia maelekezo ya kisera kwenye Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) imeelekeza asilimia 30 ya manunuzi yote ya umma ipelekwe katika kusaidia makundi ya vijana, akinamama na wenye ulemavu”amesema
Aidha amesema upo Mfuko maalumu wa kusaidia watu wenye ulemavu pamoja na mfuko wa vijana na uwezeshaji wananchi kiuchumi .
Aidha amewataka waandishi wa habari na watumishi wa umma na wadau mbalimbali kuzidi kupaza sauti juu ya uwepo wa mifuko na faida zake.
Katika hatua nyingine amezielekeza Idala na Taasisi za Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani vijana ili waweze kujua fursa za mikopo na uwezeshaji wananchi.
“Maelekezo yetu ni kwamba Idala zote , Taasisi zote kuendelea kuhakikisha kwamba elimu inakuwa ndiyo kipaumbele .. Serikali ya awamu ya sita inayoogozwa na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mambo yaliofikiwa ni pamoja na kuhakikisha watu wanapata elimu ili waweze kujinusuru katika maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Kikwete ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wote kuhakikisha wanalinda amani katika kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Octoba mwaka huu.




More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako