Na Esther Macha,Timesmajira, Online, Mbeya
Imeelezwa kuwa changamoto inayowakabili wajasiriamali kukopa fedha katika taasisi za kifedha ni uwepo wa riba kubwa, hivyo Wabunge wanaifanyia kazi ili riba hiyo ipungue.
Hayo yameelezwa leo Mei 5,2023 na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo,wakati akizindua kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Amenye Jijini Mbeya huku akisisitiza mfumo huo wa kukopa katika taasisi za kifedha utarejesha nidhamu ya urejeshaji wa mikopo ingawa changamoto itakuwa kwenye riba.
Mbunge Suma Fyandomo
Fyandomo ameeleza kuwa changamoto kubwa katika kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha ni riba kubwa hivyo kama wabunge wameliona na wanaangalia namna ya kuishawishi serikali ili kuzungumza na taasisi hizo ziweze kuweka riba ndogo ya mikopo kwa wajasiriamali.
‘’Sisi kama wabunge hili jambo tunalifanyia kazi ili tuweze kuiomba,serikali kuwa ni sawa maamuzi iliyotoa kuwa vikundi vikope kupitia benki lakini kuwe na riba ndogo kwa vikundi ili wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wasikwame kukopa fedha hizo na jambohilo linaenda kukamilika muda si mrefu ’’amesema Fyandomo.
Sanjari na hayo ameeleza sababu ya serikali ililazimika kusitisha utoaji mikopo ya asilimia 10 kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu kuwa ni baadhi ya wanufaika kutokuwa waaminifu.
Mwenyekiti wa kikundi hicho Amenye David amesema,kuwa alipata wazo la kuanzisha kikundi ambacho kilikuwa na watu 16 na kila mtu akiweka akiba ya 20,000 kwa wiki ,baada ya hapo walianza kukopeshana kwa kila mwanachama ili waweze kufanya ujasiliamali.
Kwa upande wake Mbunge Viti Maalim Zanzibar Mariam Mwinyi amesema serikali ina malengo mazuri kuona wana nufaika na mikopo huku akiwasisitiza kuwa na umoja.
‘’Mzidi kupendana katika kikundi ambacho tumekizindua tunahitaji kisonge mbele zaidi ya hapa ili muweze kujiimarisha kiuchumi katika shughuli zenu’’amesema.
More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa ushauri wa kisheria bure
CPA.Makalla atembelea miradi ya kimkakati kusini Pemba
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo