December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Hope for Girls and Women Tanzanaia, Rhobi Samwely akiwa katika usafiri wa baiskeli mara baada ya kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya ubunge kupitia NGOs Mkoa wa Mara. (Picha na Fresha Kinasa).

Rhobi Samwely arejesha fomu akiwa kwenye usafiri wa baiskeli mkoani Mara

Na Fresha Kinasa, TimesMajira Online, Mara

Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania lenye makao makuu yake Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara, Rhobi Samwely amerudisha fomu aliyochukua kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa Viti Maalumu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia NGOs katika Mkoa wa Mara akiwa na usafiri wa baiskeli.

Amesema kwamba, kuimarika kwa demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumemsukuma kuwania nafasi hiyo ili akifanikiwa atoe mchango wake katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Ameongeza kuwa, iwapo atafanikiwa atashirikiana katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ikiwemo kutetea haki za watoto, kina mama na kuendeleza kuimarisha Taifa imara chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ambaye amelipaisha Taifa kiuchumi.

Katika hatua nyingine Rhobi amebainisha kwamba, anashauku kubwa ya kutoa mchango wake kama mwanamke katika jamii iwapo atafanikiwa kuchaguliwa na chama hicho kwa maslahi mapana ya jamii nzima.

Rhobi Samwely akiondoka katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mara akiwa na dereva wake wa baiskeli aliyempeleka wakati akirejesha fomu leo.( Picha na Fresha Kinasa).

“Napongeza mafanikio makubwa yaliyotolewa na Rais Magufuli kwa muda wa miaka mitano, hakika Watanzania ametuinua kiuchumi na kutupa heshima kubwa Kimataifa, na mimi natamani mchango wangu niutoe Mungu akinifanikisha,”amesema.