March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RFB yakagua barabara ya Km 223.5 Singida–Minjingu

Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online

Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara(RFB), wametembelea na kukagua barabara yenye urefu wa kilomita 223.5 ya Singida-Katesh-Dareda-Babati hadi Minjingu,mkoani Singida.

Ziara hiyo imefanyika Septemba 18,2025, mkoani Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Mussa Natty wakiwa wameambatana na wataalamu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Singida.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara(RFB), Mhandisi Mussa Natty (wa kwanza kulia), akimsikiliza mjumbe wa Bodi hiyo,Mhandisi Alois Matei wakati RFB ikikagua barabara ya Singida – Katesh – Dareda – Babati hadi Minjingu kilomita 223.5

Ambapo wajumbe wa Bodi hiyo wamekagua hali ya barabara yenye urefu wa kilomita 223.5, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya RFB kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

Hata hivyo Singida umekuwa Mkoa wa pili ukitanguliwa na Mkoa wa Dodoma kwa wajumbe wa bodi hiyo kutembelea, kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Neema Mhondo wa kwanza kushoto akimgusia jambo Meneja wa Wakala ya Barabara(TANROADS), Mkoa wa Manyara Mhandisi Dutu Masele (wa pili kulia) wakati Bodi hiyo ikikagua barabara ya Singida – Katesh – Dareda – Babati hadi Minjingu kilomita 223.5

Wakati bodi hiyo ikiwa mkoani Dodoma,wajumbe walipata fursa ya kukagua na kujionea utekekalezaji wa matengenezo ya barabara ya Dodoma hadi Kitinku yenye urefu wa Km 66.7, uliogharimu kiasi cha milioni 911.

Aidha Bodi ya Mfuko wa Barabara itaendelea na zoezi hilo la ukaguzi katika Mikoa ya Manyara na Arusha, ili kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, katikakti,akimuelekeza jambo Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania(TANROADS),Mkoa wa Manyara Mhandisi Dutu Masele (wa pili kushoto), wakati Bodi ya Mfuko wa Barabara ikikagua barabara ya Singida – Katesh – Dareda – Babati hadi Minjingu kilomita 223.5 Wengine ni wajumbe wa Bodi hiyo