Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Namtumbo
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mradi wa REGROW imejipanga kuhakikisha kuwa wanawezesha Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) kwa kuwapatia vitendea kazi stahiki ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo katika maeneo yao ya kazi.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 22, 2023 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba wakati akifunga mafunzo ya kozi Na. 72/2023 ya Askari wanyamapori wa vijiji (VGS) katika, Chuo cha Mafunzo ya Hifadhi ya Maliasili kwa jamii Likuyu Sekamaganga, Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Aidha, Kamishna Wakulyamba, amesema Wizara inatambua umuhimu wa Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) katika kuendeleza uhifadhi na kupambana na ujangili nchini hivyo aliwasihi kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuendelea kutunza maliasili ambazo ni mojawapo ya tunu kubwa za Taifa.
Pia, amewataka wananchi wote kuzingatia maelekezo yanayaotolewa na wataalamu wa taasisi za uhifadhi ili kuepuka madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu, kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yaliyopo jirani na hifadhi.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Kamanda wa Kanda ya Mashariki, Masana Mwishawa amesema kutokana na idadi kubwa ya vijana waliochaguliwa kujiunga, mafunzo hayo yalipangwa kufanyika kwa awamu tatu (3); awamu ya kwanza yenye VGS 120 ilianza Januari na kukamilika Aprili 2023, awamu ya pili yenye jumla ya vijana 121 ilianza April na kukamilika Julai, 2023, awamu ya tatu wanahitimisha mafunzo yao vijana 113 ilianza tarehe 23 julai 2023.
Aliongeza kuwa, lengo kuu la mradi wa REGROW ni kuboresha usimamizi wa Maliasili na Utalii katika maeneo ya kipaumbele Kusini mwa Tanzania na kuwezesha shughuli mbadala za kujipatia kipato kwa jamii zinazolengwa.
Akitoa Taarifa ya Chuo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya UhIfadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga, amesema Askari 114 wamehitimu mafunzo yao wakiwemo 113 kwa ufadhili wa REGROW na mmoja (1) kwa ufadhili binafsi na kutoa wito Kwa wananchi mbalimbali kujiunga na Chuo hicho ili kujipatia taaluma adhimu ya Uhifadhi.
Matukio Mbalimbali katika picha
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi