November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Red Cross Tanzania yapongezwa kwa juhudi za usimamizi miradi ya afya

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira online,Kigoma

TANZANIA Red Cross Society imepongezwa kwa juhudi za usimamizi bora wa miradi ya afya nchini kwa kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma zilizokidhi viwango.

Akizungumza jana kwa niaba ya Serikali Kamishna wa Polisi, Nsato Marijani, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usimamizi wa Makambi na Makazi,Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wakati akikabidhi kituo cha afya cha Kambi ya Nduta kilichopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma amesema kuwa Red Cross Society imekuwa ikifanya vizuri katika usimamizi wa miradi ya afya.

Kamishna wa Polisi, Nsato Marijani, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usimamizi wa Makambi na Makazi,Idara ya Huduma kwa Wakimbizi (kushoto) akikabidhi mradi huo kwa Tanzania Red cross society nchini

“Tumeona mifano ya miradi mingine ya afya ambayo Red Cross Society ilisimamia hivyo Serikali haina wasiwasi nayo katika usimamizi wa mradi huo mpya wa afya katika kambi ya Nduta,” amesema Kamishina Marijani.

Amesema kuwa Serikali chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani inaiamini Tanzania Red Cross Society na haina mashaka nayo katika usimamizi wa mradi huo wa afya katika kambi Nduta (Nduta Refugees Camp).

Amesema kuwa Red Cross Society imekuwa ikifanya vizuri katika usimamizi wa miradi mingine ya afya nchini kama ya wakimbizi Nyarugusu na wakimbizi Mtendeli ambayo imefanya vizuri.

Amesema kuwa mradi huo umefadhiliwa na Belgium Red Cross na kuhudhuriwa na viongozi wa mashirika mbalimbali wakiongzwa na Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR),Belgium Red Cross, MSF na Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Society pamoja na wafanyakazi wapya wa TRCS wambao watafanya kazi ya kutoa huduma katika kambi hiyo ya Nduta.

MSF ambao walikuwa wanatoa huduma hiyo ya afya kabla ya Serikali kuwakabidhi Tanzania Red Cross Society ambapo pia wamekabidhi rasmi hospital hiyo kwa TRCS,Nduta cap.