January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Songwe awaonya wakurugenzi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael, amewataka wakurugenzi watendaji wa Halmashauri mkoani humo kutoingiza kiasi chochote cha fedhaa za mapato ya ndani wakati wanatekeleza miradi ya BOOST katika maeneo yao.

Pia amewataka kutumia vizuri fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu sita kwa ajili ya mradi wa BOOST kwa lengo la kuboreshaji miundombinu ya Shule za msingi.

Amesema Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 7,138,500,000 kwa ajili ya ujenzi miundombinu wa Shule za msingi 8 mpya, vyumba vya madarasa 104, pamoja na vyumba vya madarasa ya mfano kwa ajili ya elimu ya awali vyumba 10.

Pia fedha hizo zitahusika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 kwa ajili wanafunzi wenye mahitaji maalumu, matundu ya vyoo 104 na Nyumba za waalimu 2 ambazo zitachukua familia 4.

“Matarajio ya Serikali ni kuona fedha iliyokuja inakwenda kukamilisha miradi yote kwa wakati ili iendelee kuleta fedha nyingine za ujenzi wa miundombinu, kwani fedha izi ni za lipa kwa matokeo (P for R) jinsi unavyotumia vizuri ndio Serikali inakuongezea fedha kupitia mradi wa BOOST amesisitiza, Mhe. Dkt. Francis Michael.

“Serikali imeisha toa maelekezo kuwa ifikapo 30 Juni miradi yote iwe imekwisha lakini sisi hapa Mkoani tunataka kuona miradi yote ya BOOST inakamilika ifikapo 15 Juni bila kuongeza fedha yeyote kutoka mapato ya ndani” amesisitiza Mhe. Dkt. Francis Michael.

Ametaja kiasi cha fedha kwa kila Halmashauri kuwa Ileje imepata kiasi cha shilingi 1,574,100,000, Mbozi shilingi 1,700,100,000, Momba shilingi 1,114,600,000, wakati Halmashauri ya Songwe shilingi 1,039,600,000 na Tunduma TC 1,707,1000,000.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mlowo, Mwl. Denis Jimy amesema Shule yake ina imenufaika na mradi wa BOOST kwa ajili ya Kitengo cha elimu maalumu ambacho kina wanafunzi 75, tumepata fedha milioni 56 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa kwa ajili ya elimu maalumu na milioni 6 kwa ajili ya kujenga matundu 3 ya vyoo.

Naishukuru sana Serikali kwa kutuletea mradi huu wa BOOST kwani watoto 75 wa elimu maalumu wanatumia darasa moja tu kitu ambacho sio sahihi lakini sasa tumeanza ujenzi tunategemea ifikapo Juni 2023 wanafunzi wa elimu maalumu watakuwa wanasoma kwenye mazingira bora, amesema, Mwl. Denis Jimy.