November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Senyamule aliasa Baraza la wafanya LATRA

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameliasa Baraza la Wafanyakazi LATRA kuhakikisha linazingatia haki zote za msingi za wafanyakazi kama vile kulipa mishahara na stahiki zote kwa wakati.

Vile vile amewaasa watumishi wote wa LATRA kuhakikisha wanajiepusha na vishawishi vya zawadi na rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza wakati akizindua baraza la kwanza la wafanyakazi la LATRA,Senyamule amesema,vil evile amesema,baraza hilo kupitia menenjimenti yake linapaswa kuhakikisha michango ya watumishi ikiwemo pensheni ,kupandishwa vyeo kwa wakati na kwenda likizo za uzazi kwa ujibu wa sheria.

“Watumishi wote wanapaswa kupata stahiki zao zote kwa wakati na bila upendeleo na hili liatawezekana iwapo tu shughuli zitafanyika kwa kuzingatia miongozo mbalimbali iliyopo ya utumishi wa umma na kwa mujibu wa sheria.amesema Senyamule na kuongeza kuwa

“Viongozi lazima muhakikishe masuala yote ya maendeleo na matatizo ya wafanyakazi yanashughulikiwa kwa wakati ili kuondoa minong’ono na manung’uniko na hatimaye kudumisha nidhamu kazini na hivyo kuongeza ari ya wafanyakazi.”

Kwa upande Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Habibu Suluo amesema Baraza hilo jipya mkataba wake ulisainiwa Disemba 2022 na kuridhiwa Januari 2023

Aidha amesema Mamlaka hiyo imepewa jukumu la kudhibiti usafiri wa Reli ,usafiri kwa njia ya barabara ,na usafiri wa waya huku akisema kwa upande wa reli wanadhibiti reli ya kati na reli ya Tazara

Vile vile amesema,shughuli nyingine wanazopfanya ni kudhibiti usafiri wa umma kwa abiria ,maroli na kwamba wanatekeleza maukumu yao yote kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni zilizopo.