December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Mtaka:Tutaulinda Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa ili uwe alama ya Mkoa

Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema uongozi wa Mkoa utaulinda Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo ndani ya Mkoa huo ili liwe eneo litakalotembelewa na kufahamika kama alama ya Mkoa wa Dodoma.

Mtaka amesema hayo jijini hapa leo wakati alipotembelea ulipo Mnara huo eneo linalofahamika kama viwanja vya mashujaa kwajili ya kukagua maandalizi ya sherehe za maazimisho ya siku ya mashujaa zitakazofanyika Julai 25 mwaka huu huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

“Kwetu sisi kumbukumbu za mashujaa wetu ndani ya Jiji la Dodoma tunatamani eneo hili la mnara wa mashujaa liwe ni eneo ambalo litatembelewa na kuwa ni eneo ambalo litakuwa ni moja ya alama za mkoa wa Dodoma na ni moja ya eneo la kuvutia watu kwasababu ni eneo lipo katikati ya jiji hivyo nieneo zuri na linafikika kwa urahisi,

“Hivyo kwa kuanzia sisi Ofisi ya Mkoa,ofisi ya Jiji la Dodoma na Ofisi ya maadhimisho tutakutana kwa pamoja tukubaliane namna gani eneo hili litatunzwa vizuri ili liwe na faida ndani ya Mkoa wa Dodoma na kutambulika kila mahali,”amesema Mtaka

Akizungumzia maandalizi ya sherehe hizo baada ya kukagua mtaka amesema kuwa  yanaenda vizuri na kamati ya Ulinzi na usalama imeridhishwa na maandalizi hayo na iliona vyema kuja kutembelea ili hata viongozi wa Wizara wakija wakute angalau na wao kama washiriki wa kamati ya maandalizi wameshatembelea eneo la tukio.

“Sherehe za mashujaa kitaifa kwa mwaka 2022 zinafanyika Dodoma na tunamshukuru Mheshimiwa rais kwa kuona uhumimu wa mkoa wetu na kuuchagua kufanyika kwa sherehe hizi hapa Dodoma ambazo zitaanza Julai 24 usiku ambapo saa 6 usiku wa kuamkia tarehe 25 tutawasha mwenge na kuuzima usiku wa saa 6 ukiongozwa na Meya wa jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe hapa hapa katika viwanja vya mashujaa,amesema Mtaka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa maadhimisho Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bathilomeo Jungu amesema wamelikabidhi eneo lilipo mnara wa mashujaa kwa SUMA JKT ili walifanyie ukarabati kwasababu lilikuwa na hali mbaya.

“Kwasasa maandalizi yanaenda vizuri hili eneo lilikua limechoka lakini tuliwapa wenzetu wa SUMAJKT wanaendelea na ukarabati na tunashukuru ujio wa Mkuu wa Mkoa kwasababu ametupa maelekezo mengine yakuboresha zaidi eneo hili,

“Sasa hivi mafundi wanakarabati mwenge ambao utakaa pale juu na baadae wataurudisha juu kama ambavyo hua unakaa anakwenda vizuri Kutokana na kuwa eneo hilo halikuwa zuri lilikuwa limechoka na kazi ya ukarabati wamewakabidhi SUMAJKT kuhakikisha eneo hilo linakarabatiwa na kuwa katika hali nzuri,”amesema Jungu.