May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ISW yawasihi wanafunzi kujitokeza kwa wingi kujisajiri

Na Penina Malundo,timesmajira, Online

TAASISI ya Ustawi wa Jamii (ISW),imewasihi  wanafunzi wanaotaka kusoma fani mbalimbali nchini,kutembelea  banda lao katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ili kujua programu mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo mafunzo ya muda mfupi yanahusiana na changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii.

Wito huo umetolewa leo jijini humo na Naibu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Profesa Sotco Komba wakati  akizungumza na waandishi wa Habari katika maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika viwanja hivyo.

Amesema chuo hicho kina program zaidi ya 20 kuanzia ngazi ya cheti na Shahada ya Uzamili (Masters) ambapo mwanafunzi ambapo zitamfanya mwanafunzo kuchagua kusoma fani anayohitaji.

“Taasisi ya Ustawi wa Jamii tunashiriki katika maonesho haya ya Vyuo Vikuu ambayo yameandaliwa TCU, na kikubwa tunachokifanya hapa ni kuweza kuwafahamisha wanafunzi na Watanzania kwa ujumla juu ya program zetu ambazo tunazitoa,”amesema na kuongeza

“Mkishafika hapa mtakutana na vitu vingi vizuri, tutawaelekeza kuhusu program mbalimbali ambazo tunazitoa, ambazo ni pamoja na zinahusiana na mambo ya Social Work, Labour Relations  na mafunzo ya muda mfupi ambayo yanahusiana na changamoto mbalimbali ambazo jamii inakumbana nayo kwa sasa ikiwemo Stress (msongo wa mawazo) katika masuala ya kazi na changamoto za kifamilia,”amesema 

Aidha amewakaribisha Watanzania kwa ujumla kutembelea Taasisi hiyo iliyopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo pia kuna Kituo cha Elimu, Ushauri na Masuala ya kisaikolojia.

“Tunaona jamii yetu inakabiliwa na changamoto ya Sonona (msongo wa mawazo) ambapo tatizo hili limekuwa likiongezeka kila siku, kwahiyo waje kituoni kwetu kupata elimu ambayo itawasaidia na kuwarudisha katika hali yao ya kawaida ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku,” amesema Profesa Komba

Maonesho ya Vyuo Vikuu yameanza Julai 18, mwaka huu, yakihusisha vyuo vikuu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambapo yamefunguliwa rasmi jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na yatahitimishwa Julai 23, mwaka huu.