Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere, amezitaka Halmashauri zote mkoani humo, kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Makongoro ametoa maelekezo hayo Januari 07, 2025, wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wilayani Nkasi.

Miradi iliyokaguliwa wilayani Nkasi katika ziara hiyo ni ujenzi wa shule ya Amali ya Mkoa,shule mpya ya msingi Chala Chima pamoja na ujenzi wa mabweni na madarasa katika shule ya sekondari Chala.
Amesema kuwa ni jukumu la kila Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango, huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuongeza jitihada katika usimamizi wa miradi kwa kuhakikisha kazi zinaendelea usiku na mchana ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa inalenga kuhakikisha kuwa fedha za miradi ya maendeleo zinatumika ipasavyo na miradi yote inatekelezwa kwa kuzingatia muda na viwango vya ubora vilivyowekwa.

More Stories
Waziri Mkenda aeleza Tanzania ilivyoweka mikakati madhubuti Teknolojia ya Akili Unde
Polisi Mbeya yajivunia miaka minne ya mafanikio
Wahariri wa vyombo vya habari nchini wapongezwa