Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema tathimini ya Mpango wa kuwapanga vizuri Machinga Dar es salaam inaonyesha zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa Kutokana na ushirikiano mkubwa uliotolewa na Viongozi wa Machinga Jambo lililowezesha zoezi kufanyika pasipo uvunjifu wa amani.
RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao kazi Cha tathimini ya zoezi hilo ambapo amewataka Wafanyabiashara waliohama kubaki kwenye maeneo walipopangwa na sio kufanya Biashara Barabarani ambapo amesema Fursa za Mikopo ya vikundi na vitambulisho vya Machinga zitawafuata hukohuko.
Aidha RC Makalla amesema kwa Sasa Serikali inasafisha maeneo walipohama, kuboresha maeneo walipohamia na kuyalinda maeneo walipoondoka ili yasivamiwe upya.
Hata hivyo RC Makalla amesema baada ya kufanikiwa kuwapanga Vizuri Machinga kinachofuata Ni uzinduzi wa Kampeni ya Usafi na utunzaji wa mazingira Dar es salaam ambapo amewaelekeza Wakurugenzi, Maafisa Mazingira, Watendaji wa Kata na Mitaa kujiandaa kwa hilo.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19