November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC.Makalla atoa maagizo nane kutatua mgogoro mabwepande

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam,Amos Makalla ametoa maelekezo nane ya kumaliza Migogoro ya Ardhi eneo la Mabwepande Kufuatia eneo hilo kuwa kinara wa Migogoro ya Ardhi Jambo linalohatarisha usalama.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo leo wakati wa mkutano Maalumu na wakazi wa eneo hilo ambapo miongoni mwa maelekezo hayo nane ni pamoja na kuunda timu ya Wataalamu ikijumuisha Vyombo vya ulinzi na usalama, idara ya Ardhi na Wanasheria ambapo itafanya uhakiki wa nyaraka za umiliki wa ardhi kwa muda wa siku 30.kukamata Watu wote waliohusika kuuza na kutapeli Wananchi maeneo ikihusisha Wauzaji, Madalali na Wenyeviti wa Mitaa waliohusika kwenye udanganyifu.

Pia amesema manispaa ya Kinondoni kutoa elimu ya Urasimishaji wa Ardhi kwa Wananchi, kufutwa usajili kwa kampuni zote za Upimaji na Urasimishaji wa Ardhi zitakazofanya kazi kinyume na taratibu,wenye Mashamba, Mapori, Taasisi za Umma Kuyaendeleza maeneo wanayomiliki.

“Wakati kamati unafanya kazi ni marufuku Ujenzi kufanyika pasipo kibali pia alisema kuainishwa kwa Maeneo yote ya Huduma za Jamii na yalindwe yasivamiwe,”amesema

Amesema kamati kukutana na Wenye Mashamba au Mapori ambayo maeneo yao yamevamiwa ili Kuangalia njia nzuri ya busara ya kumaliza Mgogoro ikiwemo wavamizi kukubali kumlipa mmiliki halali kidogokidogo kulingana na makubaliano yao.

RC Makalla amesema anaamini njia hiyo itakuwa suluhu ya kumaliza migogoro mabwepande kwa kuwa Serikali itajua wakazi halali wa eneo hilo na kusisitiza kuwa baada ya Mgogoro kumalizika hataki kuona Mapori Mabwepande.

Aidha RC Makalla ameelekeza kusimama kwa operesheni zote za kubomoa nyumba za Wananchi mpaka hapo timu ya Wataalamu itakapomaliza kazi yake.