Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Watumishi wa Umma wakiwemo Walimu wametakiwa kufanya maandalizi bora ya kustaafu mapema kwa kuchangamkia fursa ya Mkopo kwa kuanzisha miradi ya kujikimu kwa mustakabali ya maisha ya sasa na baadae.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla katika kuadhimisha Siku ya walimu Mkoa wa Dar es Salaam na kizindua kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho – Umetufunza Tunakutunza’ chenye masuluhisho mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya Walimu Mkoani Dar es Salaam.
RC Makalla amesema Benki ya NMB ndiyo benki ambayo inatoa huduma bora na kutoa taarifa sahihi kwa wateja wake hivyo kupelekea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi alisema katika kifurushi cha “Mwalimu Spesho” kimejumuisha huduma zote zinazomuwezesha Mwalimu ikiwemo mikopo mbalimbali yenye riba nafuu ikiwemo ikiwemo ya kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake.
Mbali na mikopo hiyo, wana mikopo ya kilimo na mikopo kwaajili ya vyombo vya usafiri kama pikipiki na bajaji ambayo itawanufaisha walimu kuweza kufanya biashara inayoweza kuwaongezea kipato.
Lakini pia, Kupata mkopo wa Bima yaani Insurance Premium Finance (IPF), ambayo inawezesha Walimu kulipa bima na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali. Lakini pia, Walimu watapata mikopo ya pembejeo na Mashine za kilimo pamoja na kupata elimu ya masuala ya kifedha.
Mpaka sasa, NMB kupitia Mwalimu Spesho, imewafikia Walimu wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Kagera, Tarime na Dar es Salaam na bado wanaendelea kufikia Mikoa mingine.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati