Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Katavi.
MKUU wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,amesema kuwa upatikanaji wa maji safi na salama wa muda mrefu ni moja ya afua zinazosaidia kumaliza ugonjwa wa kipindupindu.
Hivyo amesema ni muda mwafaka kwa taasisi zinazotoa huduma za maji safi na salama kutokuwa na vikwazo juu ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi ili kuimarisha usafi unaohitaji matumizi ya maji.
Akizungumza na wanahabari Januari 01, 2025 wakati akitoa ripoti ya mpango wa serikali ya mkoa mwaka huu amebainisha uwepo wa visa kadhaa vya ugonjwa huo katika maeneo ya Kakese, Makanyagio, Magamba na Dirifu ambapo wagonjwa wamelazwa kituo cha afya Nsemlwa mjini Mpanda na wengine Karema na Ikola wilayani Tanganyika.
Akiwa katika ofisi yake, Mkuu wa mkoa huyo ameweka wazi katika usafi wa mazingira wananchi wana wajibu wa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama kuhara, kipindupindu,mafua na magonjwa ya matumbo.
“Taasisi zinazohusika na utoaji wa maji safi na salama ni Mamlaka ya maji safi na salama Mpanda (MUWASA) na Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) ambazo ni taasisi za umma zina wajibu wa kusimamia ustawi wa umma na jamii kwa kutoa huduma bora ya maji” Amesisitiza.
Mbali na kuhimiza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi ametoa rai ifikapo Januari 31, 2025 Katibu Tawala wa mkoa huo na wakuu wa wilaya za Mlele, Tanganyika na Mpanda kufanya ukaguzi wa kina na misako katika mitaa na vijiji hususani kwenye maeneo ya biashara, masoko na migahawa.
“Naniwapa mamlaka kwamba mkigudua kuna eneo linahatarisha usalama wa afya za wanakatavi chukueni hatua za kisheria bila kupepesa macho panapositahili kufungwa kwa mujibu wa sheria pafungwe ili marekebisho yaweze kufanyika”amesema.
Mrindoko vilevile amewagiza wakuu wa wilaya kuchua hatua kwa timu za wataalamu kutoa elimu na kuhimiza matumizi ya vyoo na uwepo vya vyoo na matumizi ya maji salama yaliyochemshwa.
Serikali imeendelea kufanya juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu katika mikoa ambayo imeripotiwa kuwa na ugonjwa huo kwa kupeleka vifaa tiba na dawa ya kutibu maji takribani milioni saba ili kuendelea kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu nchini.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
HAYA HAPA MATOKEO YOTE FORM II NA DARASA LA IV
Ufaulu waongezeka matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili