Na Heri Shaaban,TimesMajira Online,Dar
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amekerwa na migogoro ya ardhi ya Jimbo la Kawe na Kinondoni imechukua muda mrefu bila ufumbuzi wake .
Mkuu wa Mkoa Makalla ameyasema hayo katika siku ya kwanza ya ziara yake kwa Mkoa wa Dar es Salaam ya kutembelea majimbo ya Mkoa huo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi
“Kata ya Kawe ni nyumbani kwangu nimeshawai kukaa leo nimeacha ofisi yangu nimeanza ziara ya kutatua kero za wananchi katika Mkoa huu Jimbo la Kawe na Kinondoni linaongoza kwa mgogoro ya ardhi ” amesema Makala.
Makalla amesema hajafurahishwa na migogoro hiyo ambayo migogoro mingine inachangiwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya hiyo wakiiipa Serikali hasara Chasimba ,Chasamba na Mabwepande amewataka wananchi kuandaa vielelezo vyao Mara baada ziara yake ya Mkoa kumalizika atakwenda na Waziri wa Ardhi William Lukuvi kutatua migogoro ya Ardhi .
Makalla amesema katika ziara hiyo amefurahishwa kumkuta Mbunge wa Jimbo la Kawe jimboni Josephat Ngwajima kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo hilo.
Akizungumzia Maendeleo ya Jimbo la Kawe Mkuu wa Mkoa Makala alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Hassan Suluhu imetenga shi bilioni 24 kwa ajili ya Barabara za Zege ,na za kiwango cha lami na Changalawe ,sekta ya maji shilingi bilioni 65 wananchi wataunganishiwa maji kutoka Ruvu .
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Makalla amemwagiza Afisa TAKUKURU ,Afisa Ardhi na Mkuu wa Wilaya hiyo kuanzia kesho Agosti 31 /2021 kufatilia migogoro ya ardhi ya Jimbo hilo kufuatia wananchi kuvunjiwa nyumba zao na mmiliki wa eneo hilo ambalo wananchi wanadai walilipa fedha benki milioni 15 kila mmoja bila kuwandikishiana .
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewagiza Madiwani wa Mkoa Dar es Salaam ,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Maafisa Watendaji wa Kata kufufua Ulinzi Shirikishi katika Kata zao na kuimalisha ulinzi na Usalama.
Kwa upande wake Mbunge wa Kawe Josepht Ngwajima amesema Jimbo la Kawe lina Kata kumi changamoto,Barabara, maji ya Dawasa,mafuriko ,vijana kukosa ajira wa Jimbo hilo.
Changamoto zingine Mbunge Ngwajima amesema Wananchi kubomolewa bila kulipwa,Mikopo ya Serikali kwa vikundi vya Wanawake na Watu wenye ulemavu pamoja na Wanafunzi kutembea umbali mrefu.
More Stories
Wahakikishiwa usalama siku ya kupiga kura
CCM inabebwa na kazi nzuri za Rais Dkt. Samia-Makalla
Wananchi Babati wamshukuru Rais Samia kwa kuwafungulia barabara