Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
MKUU wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Albert Chalamila, amewataka watanzania kuwa na imani na Jeshi la Polisi kwa kipindi hiki wakiendelea na uchunguzi juu ya waliotekeleza shambulizi la Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC) Padri Charles Kitima.
Chalamila, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es- Salaam,kulaani tukio la kushambuliwa
kwa Padri Kitima,amesema wapo walio na mashaka na taarifa ambayo imetolewa na Jeshi la Polisi,hivyo amewaomba waeendelee kuwa na usikivu na wale ambao wameonesha mashaka wawe na imani kwa kuwa vyombo vya dola havitamuonea yeyote.
“Rai yangu mjenge imani kwa vyombo vya dola kwamba jambo hili litafika mwisho na aliyefanya atabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria,”amesema Chalamila.
Pia ametoa wito kwa Watanzania kuachana na dhana ambayo inaenezwa ikiihusisha Serikali pamoja na maasula ya kisiasa katika tukio hilo la kushambuliwa Padri Kitima.Kwani Tanzania ni nchi ya sheria hivyo wavute subira na watulie kupisha uchunguzi wa tukio.
Aidha amesema,tukio alilofanyiwa Padri Kitima linaweza kumkuta mtu yoyote hivi karibuni hata yeye lilimkuta maeneo fulani watu walitaka kumpora simu lakini walishindwa kwa sababu alikuwa na ulinzi mwisho wale watu wakakamatwa wote.
More Stories
AAFP yampitisha Ngombare Mwiru kugombea Urais Bara
DC Mpogolo:DMDP kujenga barabara za urefu km 67 Ilala
Uhakiki na uchambuzi wa kazi za waandishi wa tuzo za Samia Award wafanyika kwa weledi