March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Chalamila atoa maagizo kwa viongozi wa mkoa, wataalamu kufuatilia kuondoa changamoto mbalimbali

Na Bakari Lulela,Timesmajira

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ametoa maagizo kwa viongozi wa mkoa na wataalamu kufuatilia kwa kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo kwenye maeneo ya bandari yanayosababisha msongamano na ufinyu wa Barabara. ikiwemo ujenzi holela

Pia amesema watendaji wa bandari kwa kushirikiana na viongozi kuwa wabunifu kwenye kulifanya jiji linakuwa kivutio cha wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es salaam, na wakuu wa wilaya za kigamboni , Ilala na Temeke sambamba na watendaji wakuu wa bandari kwenye Ofisi za mkurugenzi wa Mamlaka hiyo mkuu wa mkoa alisema bandari ndio kitovu cha uchumi nchini inatakiwa kuiangalia kwa macho mawili.

“Bandari ya Dar es salaam inatajwa kuwa ni bandari kongwe na yenye fursa kubwa kwa uchumi wa nchi hivyo suala la msongamano na foleni sambamba na ujenzi holela wa hoteli zenye hadhi huweza kudholotesha uchumi wa nchi yetu,” amesema Chalamila 

Aidha Chalamila amewataka Mamlaka husika ikiwemo Tanroad na Tarura kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Barabara Ili waendao kwa miguu na maegesho ya magari yasiweze kuingiliana na barabara kuu ambayo hupitishia mizigo ama kontena kutoka eneo moja kwenda lingine.

Aliendelea kusema kuwa pembezoni mwa barabara itokayo kwenye kiwanja cha ndege kiweze kupanda Maua ili kuwa kivutio cha wageni watokao nje na kuingia jijini hapa.

Kwa upande wake mkuu wa Ilala Edward Mpogolo ameipongeza hatua hizo na kuahidi kupokea maagizo ya kushirikiana na wataalamu katika kuboresha maeneo ya bandari ikiwemo kuondoa ujenzi holela wa majengo yasiyo rasmi yaliyoko pembezoni mwa Barabara.

“Napongeza jitihada hizo lakini napokea maagizo haya ambapo naahidi nitashirikiana na wataalamu katika kuboresha wa eneo la bandari na jijini hili kwa ujumla wake.”alisema Mpogolo 

Mpogolo alisema Ili kufanikisha jitihada za serikali kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassani ya kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa lango la kibiasha hapa nchini kwetu na nje ya nchi ni kuhakikisha Barabara zinazoingia katika bandari yetu zinapitika kwa urahisi. 

Mwakilishi wa bandari Mkurugenzi Meleck Shange ameeleza kuwa wamekuwa na uboreshaji wa bandari ambapo wapo katika uwajibikaji na hatua mbalimbali na wataendelea kupambana na kuhakikisha wanayafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa.