December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ray C amchana Mwijaku

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki w Bongo fleva mwenye makazi yake kwa

sasa Ufaransa Rehema Chalamila maarufu kama ‘Ray C’

amemchana Mwijaku kuhusiana na Bongo Fleva.

Akimpa makavu hayo Kupitia kwenye ukurasa wake wa

instagram, Ray C amepost video clip ya msanii Ruby

akiimba, huku akiuliza; “Nani kasema Tanzania hakuna

vipaji?.

“Bongo Flava iko damuni na nitaipenda na kuitetea daima

maana ndio muziki ninaousikiliza miaka yote hata kama

siko Bongo!.Sema nini, Mwijaku unatulisha matango

mchana kweupee, kama mnawaza Grammy basi itakuwa ndoto

kama wasemaji na wainuaji wa vipaji wa sasa ni

Mwijaku… Rest in Peace Ruge Mutahaba.

“Unamsikitisha sana huko aliko, maana umetokea mikononi

mwake na unaujua muziki vizuri sema unaleta ukatuni!.

Poa basi Fanya ziara ya studio mbaliimbali hapo

Tanzania kama kweli una nia ya kuinua vipaji vya

ukweli maana vimejaa mitaani huko najua wajua na

nyumbani kwako THT kuna watoto walioachwa njia panda

baada ya bosi kuondoka na unajua kabisa wana vipaji vya

kuzaliwa wanahitaji kusikika kupitia hiyohiyo media

ambayo aliekufanya uwepo hapo hayupo leo.

“Najua kwako kutrend ni fahari ila unawakosea sana

vijana wenye vipaji vya ukweli. Unajitoa akili

kutulisha mpunga wakati ndani ya nafsi yako unajua

unapuyanga. Unatulisha matango,” amesema Ray C.