Na David John, TimesMajira Online
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametaka Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam umebadilishwa jina na sasa utaitwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Rais Magufuli ameyasema hayo Leo, Julai 28, 2020 wakati akitoa hutoba kwenye misa ya mwisho ya kumuaga Benjamini William Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Amesema, kuanzia jana amepokea ujumbe mwingi na mapendekezo ya uwanja huo kubadilishwa jina ikiwa kama njia moja wapo ya kumuenzi kiongozi huyo ambaye alikuwa shabiki wa klabu ya Yanga.
Amesema kuwa, ingawa kiongozi huyo hakupenda vitu kuitwa kwa jina lake lakini hakuna jinsi kwa hilo la uwanja kwani ni lazima utaikwa uwanja wa Mkapa.
“Nimepata meseji nyingi kwamba uwanja huu wa Taifa uliopo mbele yetu uitwe jina lake, na mimi natamka rasmi kuwa kuazia leo uwanja huu utaitwa Benjamin Mkapa Stadium, ” amesema Rais Magufuli.
Jana Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji alianzisha maombi aliyoyaelekeza kwa Dkt. Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja huo kuwa wa Benjamin William Mkapa.
Katika maombi hayo, uliwaomba Watanzania wote bila kujali ushabiki wa klabu waunge mkono kwa kuweka sahihi ili kumuomba rais akubali ombi hilo.
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes