ATLANTA,Marekani
MSIMAMIZI mkuu wa timu ya Kikapu ya Hawks Atlanta
Schlenk, ameamua kumpa ukocha mkuu Nate McMillan baada ya kufikia makubaliano kufuatia timu hiyo kufanya vyema msimu huu wa Ligi Kuu ya Kikapu Marekani NBA, na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.
Mpango huo umekuja, baada ya McMillan,kuiongoza timu hiyo kutinga fainali huku
Schlenk akisema makubaliano yalifikia muahafaka mapema na kocha huyo huyo kukubali kuiongoza Hawks katika mchezo wa fainali utakaopigwa kesho Jumatano pamoja na kuimarisa kikosi msimu ujao.
McMillan, mwenye umri wa miaka 56, aliteuliwa kuwa kocha wa mpito baada ya Lloyd
Pierce alipofutwa kazi wakati timu hiyo ilipokuwa na rekodi ya 14-20. Hawks walifurahia mabadiliko ya mara moja chini ya McMillan.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania