December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rasilimali za Nishati kuendelea kuboreshwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

SERIKALI imeahdi kuendelea kuboresha rasilimali za nishati za ndani ambazo zitapunguza gharama na kukuza bei ya nishati, hali itakayoongeza utegemezi wa nishati na kuongeza ufanisi wa katika kukuza pato la mtanzania mmoja mmoja na la taifa kwa ujumla.

Hayo aliyasemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba kwenye Kongamano la Wadau wa Gesi
ya LPG Afrika Mashariki 2023.

Mhandisi Mramba alibainisha kuwa
maonyesho hayo yatasaidia kukuza
ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza
sekta ya nishati nchini.

“Bila shaka kongamano hili litakuwa
jukwaa muhimu katika kuongeza uelewa
na kukuza uwekezaji katika sekta ya
nishati hasa katika sekta ya LPG nchini
Tanzania.

“Ni dhahiri kwamba mkusanyiko huu pia utawezesha wadau wote wakuu
wa sekta ya LPG kujadili maoni yao na
kushiriki masuala ya hivi punde kuhusu
mitindo ya biashara ya LPG nchini na
duniani kote,” alisema.

Alisema kuwa serikali inatekeleza
majukumu yake kikamilifu katika
kuhimiza utunzaji wa mazingira na afya
za Watanzania kwa kutoa elimu hali
inayosaidia kupunguza matumizi ya
kuni na kuhimiza matumizi ya LPG kama
nishati mbadala ya kupikia majumbani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa LPG Tanzania, Amos Mwansumbue
alisema asilimia kubwa ya mitungi ya
gesi tunayotumia inatoka nje, bado
hakujawa na viwanda vya kutosha vya
kuzalisha mitungi hiyo, hivyo wadau
kutoka nje ambao wanajishughulisha
na utengenezaji wa mitungi hiyo
wamealikwa katika kongamano hilo
kuja kushiriki na kuleta ujuzi zaidi wa
mitungi hiyo.

Maonyesho hayo yanahusiana na biashara ya LPG, ambapo Kongamano
hilo limeratibiwa na Kampuni ya LPG
Expo kutoka Singapore.

Watu kutoka nchi mbalimbali
wamealikwa ambao wanajihusisha
na biashara ya LPG duniani kote
wakiwemo watengeneza mitungi ya
gesi kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo
Japan, Indonesia, Uturuki.

Aidha, alisema katika kongamano hilo kuna waelimishaji ambao wamekuja
kuwaelimisha Watanzania kuhusu gesi
yenyewe ya LPG kwa kutoa mifano
mbalimbali kutoka nchi tofauti duniani.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Taifa ya Gesi, Hamisi Ramadhani alisema katika maonyesho hayo wanapata nafasi ya kuangalia teknolojia mbalimbali zilizopo ambazo zinaweza zikatumiwa na makampuni vile vile na wananchi kuweza kuendeleza matumizi endelevu ya gesi.

Aidha, alisema ni fursa kwao kushiriki mjadala ambapo wanabadilishana mawazo namna ambavyo wanaweza wakakuza matumizi ya gesi nchini ili kuweza kuachana na madhara ya matumizi ya mkaa na kuni.