Na Mwandishi wetu Timesmajira online
KATIKA kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita iliyopo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Taasisi isiyoyakiserikali inayojiusha na kuiwezesha jamii ipate huduma binafsi za kijamii, Raoma Foundation imezindua kampeni ya Twenzetu darasani 2024 iliyolenga kuamasisha jamii na wadau kushiriki kuchangia maendeleo ya wanafunzi shuleni.
Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa kampeni hiyo Mwanzilishi wa Taasisi ya Raoma Foundation, Rahma Mohamed amesema kupitia mradi huo wamelenga kuwafikia watoto 4509 wenye mahitaji mbalimbali.
Rahma amesema wameamua kuja na mradi huo ili kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita katika jitihada za kuhakikisha elimu inapatikana bure yenye ubora kwa manufaa ya wananchi wote.
Amesema kampeni hiyo
itaendeshwa Kwa kipindi Cha mwaka mzima wa 2024 nchi nzima ambapo kwa mikoa ya awali itakayonufaika na mradi huo ni Dodoma, Lindi, Mtwara,Singida, Kigoma pamoja na Akizimkazi Zanzibar.
“Kupitia mradi huu tumelenga kuwafikia watoto 4500 katika Mikoa hii wenye mahitaji kwani mafanikio ya mtoto darasani yanaanza na Mimi na wewe,”amesema Rahma.
Aidha amesema kupitia kampeni hiyo wamelenga kuwapatia watoto mahitaji ya kuanzia nguo zake za shule, madaftari, penseli, madaftari pamoja na kumrekebishia mazingira anayosomea.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa mradi huo, Sixtus mapunda ameipongeza Taasisi hiyo kuja na mradi huo ambao utawasaidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu.
Amesema Serikali inatambua mchango wa Taasisi hiyo kwa kuiunga mkono kwa kutoa fursa ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
“Kwenye elimu ndo kuna kila kitu kwani imekuwa ikisaidia kumuwezesha mtu kuaminiwa na kumuongezea mtu kujiamini,”amesema.
Balozi wa kampeni hiyo, Tabu Mtingita amesema wamejipanga kupita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha mtoto ambaye amekuwa akishidwa kupata elimu bora anakaa darasani na kupata masomo yake vizuri.
“Kupitia Taasisi ya Rauma Foundation tumejipanga na tutakuwa begabega kufika katika mikoa husika ili kuhakikisha mtoto anasimama na kupata elimu bora,”amesema.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam