Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri, Premier Bet, imemtangaza mshindi mpya Athumani Ramadhan aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 48,120,656, baada ya kuweka mkeka wa timu 12 kwa dau la shilingi 900 tu.
Mshindi huyo alitangazwa jana na Meneja Masokowa Premier Bet Tanzania, Eric Kirita, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.
Kirita alisema, wanajivunia kuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya Athumani Ramadhani na wanamshukuru kuendelea kuwa mteja wao.
“Ushindi huu unaonyesha jinsi Premier Bet, inavyotoa nafasi kubwa kwa wateja wetu kujishindia zawadi kubwa na kupata furaha isiyo na kifani,” alisema.
Aidha, alisema wamekuwa wakizingatia umri kwa watu wanaocheza mchezo huo wa kubashiri ambapo mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 haruhusiwi kushiriki.
“Katika kuhakikisha kubashiri kunafanyika kistaarabu na kwa mujibu wa kanuni na sheria michezo ya kubahatisha, Premier Bet inatambua umuhimu wa kudhibiti upatikanaji wa huduma zetu kwa watu walio na umri unaostahili. Kwa hiyo, ni sera yetu kutoa huduma za kubashiri kwa watu walio na umri wa miaka 18 na zaidi tu,” alisema.
Pia, alisema wamekuwa wakiwapa ushauri wa kifedha wateja wao kutokana na utashi na sera zao ili kuhakikisha fedha wanazozipata ziweze kuzaa matunda.
Kirita, aliendelea kuwakumbusha wananchi kuhusu promosheni yao ya “Premier Bet Cash” ambapo wateja wao wanapata nafasi ya kujishindia 800,000/- kila Ijumaa kwa kujisajili na Zone Gold kupitia tovuti yao ya zonegold.com.
“Hii ni fursa nzuri ya kuongeza uzoefu wako wa kubashiri na Premier Bet.”Alisema
Kwa upande wake Afisa Mkaguzi Mkuu Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Juhudi Ngolo aliwataka watanzania kuhakikisha wanajikita katika shughuli halali za kiuchumi na kubeti iwe ni sehemu ya ziada na kuwaasa washindi wote kutumia fedha wanazozipata kujikwamua kiuchumi.
Naye mshindi huyo, Athmani Ramadhani aliwashukuru Premier Bet kwa kumpa ushindi na ameahidi fedha hizo kwenda kuziongezea kwenye biashara zake ndogondogo anazozifanya Kila siku.
“Mimi ni mfanya biashara ndogondogo, nimepata fursa hii nitaongezea kwenye biashara yangu lakini pia sitomsahau mama yangu mzazi”
Athman aliwataka watu wote wanaotaka kucheza na wanaoendelea kucheza mchezo huo wa kubashiri, wasikate tamaa na waendelee kubashiri na Premier Bet kwani kampuni hiyo ni ya kuaminika zaidi.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania