*Amesema matarajio yake ni kufika mbali kwa uwezo wa Mungu
*Awasisitiza wanaCCM kuchangia harambee hiyo
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Dar
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameichangia kiasi ch shilingi milioni 100,katika harambee ya kukusanya kiasi cha bilioni 100 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kampeni za chama hicho zinazotarajiwa kuanza Agosti 28, mwaka huu.
Akisisitiza kuwa matarajio yake ni kufika mbali huku akiwahimiza wanaCCM,wadau na wananchi kukichangia chama hicho fedha kwa ajili ya kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Rais Dkt.Samia ameyasema hayo Agosti 12, 2025,kwenye harambee ya kukichangia chama hicho, fedha kwa ajili ya kusaidia kwenye shughuli za kampeni zinazotarajiwa kuanza Agosti 28, mwaka huu. Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-Salaam.
“Nimejipanga vyema kuelekea katika uchaguzi mkuu,na chama pia kimejipanga vyema.Kwa dhati ya moyo wangu natarajia kufika mbali kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu,niwaombe wana chama wa CCM mjitoe kwa kuchangia, na nina amini wanachama wote watajitoa kuchangia,”amesema Dkt. Samia.


“


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako