Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa yatakayofanyika Julai 10 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu maadhimisho hayo ,Waziri Bashungwa amesema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajia kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha amesema Wizara hiyo kupitia JKT linaendelea kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la Kuibua na kuendeleza vipaji kwa vijana walio katika makambi mbalimbali hapa nchini vitakavyowawezesha kujiajiri
” Moja kati ya maagizo ya Rais Samia kwa JKT ni kuibua, kulea na kukuza vipaji vya vijana wa JKT ,nasi tunaendelea kutekeleza agizo hilo na siku ya maadhimisho hayo tutajionea vipaji kutoka kwa vijana hao.”amesema Waziri Bashungwa.
Kwa mujibu wa Waziri Bashungwa katika sherehe za maadhimisho hayo ya JKT yatapambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na gwaride Maalum.
Aidha pamoja na mambo mengine, maadhimisho hayo yalitanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya miaka 60, ambao ulizinduliwa na Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango kwenye makao makuu ya JKT Chamwino jijini hapa lakini pia uzinduzi wa maonyesho ya shughuli na huduma mbalimbali zinazofanywa na JKT ambayo yanaendelea katika viwanja vya SUMAJKT House jijini Dodoma.
Pia JKT liliwatembelea wahitaji hospitali na kutoa msaada katika kituo cha malezi ya watoto Kikombo jijini Dodoma.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto